A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, September 19, 2020

WAKALA WA VIPIMO (WMA) YAZUNGUMZIA MAFANIKIO YA MASOKO YA DHAHABU.

 IMG_6937


IMG_6934

IMG_6925

IMG_6910

IMG_6902

OFISA Vipimo Mkoa wa Geita, Chrispinus Aloyce amemshukuru Rais Dkt John Magufuli kwa kuweza kusogeza huduma zinazohusu biashara ya madini karibu na wananchi.

Amesema kuwa Geita imebarikiwa kuwa na maeneo mengi ya uchimbaji wa madini pia masoko ya madini hayo ya dhahabu.

Aloyce ameyasema hayo leo katika viwanja vya maonyesho ya madini yanayoendelea mkoani humo wakati Akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu wao sababu za kushiriki maonyesho hayo.

"Tunamshukuru Rais Dkt Magufuli kwa kutusogezea karibu huduma ya biashara hii ya madini na ukizingatia Geita ina masoko tisa ambayo ni Geita mjini, katoro, nyang'hwale, Mbogwe, pamoja na maeneo mengine ndani ya mkoa wa Geita" amesema Aloyce

Ameongeza kuwa wao kama wakala wa vipimo kazi yao kubwa kukagua na kuhakiki mizani ambapo wafanyabiashara wasiwe na wasiwasi kwani mizani yote inayotumika kupima madini imeshahakikiwa na ipo salama.

"Tunawaalika wadau mbalimbali kutembelea kwenye banda letu kwani Kuna mambo na kama wanakutana nachangamoto zinazohusu vipimo basi wasisite kutembelea Ofisi za wakala wa vipimo popote Tanzania" amesema.

Paulus Oluochi amesema wanapatikana wakati wote kwa mawasiliano ya 0800 11 00 97 ambapo namba hizo zinapigwa bure .

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages