A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, September 9, 2020

VODACOM TANZANIA PLC YAWAJENGEA UWEZO WA MASOMO YA SAYANSI WANAFUNZI WA KIKE NCHINI

  • Yadhamini mafunzo ya 'Women in Data Science 2020' yaliyowashirikisha wanafunzi kike wa shule za sekondari kutoka maeneo mbalimbali nchini
Mkurugenzi wa Rasilmali Watu, Vodacom Tanzania Plc, Vivianne Penessis (kulia) akiongea na wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari wakati wa kuhitimu mafunzo ya kuwajengea uwezo wasichana katika masomo ya sayansi (Women in Data Science) Dar es Salaam 2020 yaliyoandaliwa na Tanzania Data Lab (DLab) kwa udhamini wa Vodacom Tanzania Plc.(#Codelikeagirl) Kushoto ni Mkurugenzi wa Tanzania DLab Stephen Chacha. Jumla ya wasichana 60 walihitimu mafunzo hayo ya muda mfupi.

Mkurugenzi wa Rasilmali watu, Vodacom Tanzania Plc, (HR) Vivianne Penessis (kulia) akimkabidhi zawadi ya begi Loyce Nasoro wa kundi la Solveit kwa kuibuka mshindi wa tatu wa ubunifu wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wasichana katika masomo ya sayansi (Women in Data Science) Dar es Salaam 2020 yaliyoandaliwa na Tanzania Data Lab (DLab) kwa udhamini wa Vodacom Tanzania Plc.(#Codelikeagirl). Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa DLab Stephen Chacha. Jumla ya Wasichana 60 walihitimu mafunzo hayo ya muda mfupi.
Mkurugenzi wa Rasilmali watu, Vodacom Tanzania Plc, Vivianne Penessis (kulia) akimkabidhi zawadi Nilham Ally wa kundi la Soko Poa baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa ubunifu wa tovuti inayoonesha namna ya kuuza na kununua bidhaa za vyakula wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wasichana katika masomo ya sayansi (Women in Data Science) Dar es Salaam 2020 yaliyoandaliwa na Tanzania Data Lab kwa udhamini wa Vodacom Tanzania Plc.
Mkurugenzi wa Rasilmali watu, Vodacom Tanzania Plc, Vivianne Penessir (kulia) akimkabidhi Rayyan Ahmed cheti cha kuhitimu mafunzo ya kuwajengea uwezo wasichana katika masomo ya sayansi (Women in Data Science) Dar es Salaam 2020 yaliyoandaliwa na Tanzania Data Lab (DLab) kwa udhamini wa Vodacom Tanzania Pllc. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa DLab Stephen Chacha. 



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages