Balozi wa Indonesia kwenye Umoja wa Mataifa, ambaye nchi yake ndiyo mwenyekiti wa zamu wa Baraza la Usalama, amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya wajumbe walio wengi kupinga juhudi hiyo ya Marekani dhidi ya Iran.
Mataifa mengine wanachama wa Baraza la Usalama isipokuwa Jamhuri ya Dominica yamesema pendekezo la Marekani ni kinyume na sheria kwa sababu nchi hiyo ilijitoa kwenye mkataba wa nyuklia na Iran mwaka 2018.
Alhamisi iliyopita waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Mike Pompeo alisema pendekezo la nchi yake lina msingi wa kisheria licha ya Marekani kujitoa kwenye mkataba wa nyuklia kati ya Iran na madola sita yenye nguvu.
No comments:
Post a Comment