A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, August 14, 2020

RC KUNENGE AMUAPISHA MKUU MPYA WA WILAYA YA ILALA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge akimuapisha Mkuu mpya wa Wilaya ya Ilala Bw. Ng'wilabuzu Ndatwa Ludigija alieteuliwa hivi karibuni na Rais Dkt. John Magufuli kuongoza Wilaya hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge akisaini Waraka wa Kiapo mara baada ya kumuapisha Mkuu mpya wa Wilaya ya Ilala Bw. Ng'wilabuzu Ndatwa Ludigija alieteuliwa hivi karibuni na Rais Dkt. John Magufuli kuongoza Wilaya hiyo.

Mkuu mpya wa Wilaya ya Ilala Bw. Ng'wilabuzu Ndatwa Ludigija akiapa kuitumikia Wilaya hiyo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge.
Mkuu mpya wa Wilaya ya Ilala Bw. Ng'wilabuzu Ndatwa Ludigija akisikiliza kwa makini maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge (hayupo pichani).
Wakuu wa Wilaya Tano za Jiji la Dar es Salaam katika Picha ya Pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amemuapisha Mkuu mpya wa Wilaya ya Ilala Bw. Ng'wilabuzu Ndatwa Ludigija alieteuliwa hivi karibuni na Rais Dkt. John Magufuli kuongoza Wilaya hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo RC Kunenge amewaelekeza Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia ipasavyo suala zima la ukusanyaji wa mapato na matumizi ya fedha za serikali pamoja na kusimamia suala la Mazingira.

Aidha RC Kunenge amewataka wahakikishe wanaboresha mazingira ya uwekezaji huku akiwataka watumishi wa Mkoa huo kufanya kazi kwa ushirikiano kama timu ili kwa pamoja watatue kero za wananchi.

RC Kunenge pia amewahimiza Wakuu wa Wilaya kusimamia suala la Ulinzi, Usalama na Amani hususani kipindi hiki ambacho Taifa linaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Ng'wilabuzu Ndatwa Ludigija ameeleza kuwa ataenda kusimamia ipasavyo utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na utatuzi wa kero mbalimbali za wananchi wa Wilaya hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages