A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, August 21, 2020

MTENDAJI AKALIWA KOONI KWA KUSHINDWA NA KASI YA RAIS KULETA MAENDELEO

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Jokate Mwegelo(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kisopwa baada ya kufika shuleni kwa ajili ya kuzungumza na wananchi baada ya kukagua miundombinu ya shule hiyo.

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Jokate Mwegelo ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Wilaya hiyo kumbadilisha Mtendaji wa Kijiji cha Kisopwa Barabarani kwani ameshindwa kwenda na kasi ya Rais Dk.John Magufuli katika kuwatumikia wananchi na kushughulikia changamoto zao.

Jokate amesema hayo wakati anazungumza na wananchi wa Kijiji cha Kisopwa baada ya kwenda kukagua shule ya Msingi kisopwa ambayo miundombinu yake ya choo imeharibika na tayari Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe imetanga Sh.milioni 8.8 kwa ajili ya kutengeneza choo kipya cha shule.

Akiwa na wananchi hao alipata malalamiko ya kwamba baadhi ya viongozi wa kijiji hicho akiwemo Mtendaji wa Kijiji na Mwenyekiti wao wamekuwa wakikwamisha maendeleo kwa kutoshiriki kwenye vikao vya wananchi.
Jokate Mwegeleo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani akisisitiza jambo wakati anazungumza na wananchi wa Kijiji cha Kisopwa wilayani humo.

Kutokana na malalamiko hayo ndipo Jokate akaeleza kwamba "Lazima Kisopwa ipate viongozi wanaoendana na kasi ya Rais wetu Dk.Magufuli katika kutatua kero, na kufanyia kazi maelekezo ambayo yanatolewa.

"Sasa tukiwa na viongozi ambao hawawezi  kuendana na kasi na kuhudumia wananchi hao viongozi hawatufai.Ndugu zangu kuna mambo mengi sana Serikali inafanya juu yenu lakini tusipokuwa na viongozi wa kufuatilia na kusimamia hayo mambo watakwama.

"Kuna bomba la maji limepita hapa Kisopwa na DAWASA wamekuja zaidi ya mara tatu lakini wakifika hapa viongozi hawapo.Najiuliza viongozi wa hapa wanafanya nini?Wanauza sura, sawa uza sura lakini fanya kazi. Nikasema huyu kiongozi wa hapa  lazima abadilishwe".
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo akiwa na viongozi wa idara ya elimu Msingi wilayani humo wakikagua miundombinu ya choo cha Shule ya Msingi Kisopwa ambayo imeharibika baada ya kutitia.

Amefafanua wananchi wa Kisopwa wanajitahada kubwa katika kufanya maendeleo na hawana shida lakini shida iko kwa viongozi."Huwa nasema bora shida iwe kwa wananchi sio viongozi.Inasikitisha kiongozi kuwa sehemu ya changamoto".

Jokate amesema hafurahishwi na utendaji kazi wa viongozi hao na hivyo lazima ufanyike utaratibu wa kuwaondoa kijijini hapo na kuwapeleka kwingine.

Kuhusu ujenzi wa choo cha shule ya Kisopwa ambacho kwa sasa kimetitia, Jokate amesema amewapa pole kwa changamoto ya miundomboni ya shule ya msingi Kisopwa lakini anashukuru ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya ya Kisarawe tayari imekwisha tenga Sh.milioni 8.8 kwa ajili ya kujenga vyoo vipya.
Miundombinu ya choo cha Shule ya Msingi Kisopwa kinavyoonekana kwa sasa baada ya kuharibika.

"Nataka kijengwe choo cha kisasa, fedha tayari zimekuja na wananchi naomba muwe sehemu ya kusimamia fedha hizi.Tuwe na choo chenye kiwango hapa Kisopwa.Lakini pia mbali ya ujenzi wa choo, hapa lazima tujenge madarasa mapya ya Shule ya Msingi Kisopwa na mimi nitachangia mifuko ya saruji 50 kwa ajili ya ujenzi wa mdarasa mapya,"amsema Jokate.

Amefafanua kuwa Rais Dk.John Magufuli amekuwa akieleza kila siku kuwa Tanzania itajengwa na Watanzania wenyewe na ndivyo hivyo hivyo inavyotakiwa kufanyika kwa ngazi ya vijiji na vitongoji kwamba wananchi wawe wa kwanza kushiriki kuleta maendeleo yao na kisha Serikali kusaidia pale ambapo wananchi wameishia.

"Tusisubiri misaada kutoka nje, na hii ni sawa sawa na kwenye vijiji na vitongoji maendeleo lazima yaanze na sisi wenyewe, Mkuu wa Wilaya na Halmashauri inakuja kuchangia yale ambayo ninyi mmenza kufanyanya, kwa hiyo hili la vyoo kuna Sh.milioni 8.8 ,pale nikute matundu ya vyoo ya kisasa, mfumo mzuri ambao utadumu.

"Maelekezo mengine itafutwe fedha kwa ajili ya kujenga madarasa mapya katika eneo hilo la Kisopwa. kampeni ya tokomeza Zero Kisarawe sote tunaifahamu , hivyo lazima tuweke juhudi katika kuboresha miundombinu ya shule yetu hii,"amesema.
Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Kisopwa wakiwa makini kumsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Jokate Mwegelo wakati anazungumzia changamoto ya baadhi ya viongozi wa kijiji hicho kushindwa kutekeleza wajibu wao kwa wananchi.
Mafundi wakiendelea na kazi ya kuchimba shimo kwa ajili ya ujenzi wa choo kipya katika Shule ya Msingi Kisopwa ambapo sh.milioni 8.8 znatarajia kutumika katika ujenzi wa choo hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegeleo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kisopwa.
Baadhi ya wananchi wa Kisopwa wakimuaga Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo baada ya kuzungumza nao kuhusua masuala mbalimbali ya maendeleo.
Miundombinu ya choo cha Shule ya Msingi Kisopwa kinavyoonekana kwa sasa baada ya kuharibika.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages