Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
Manispaa ya Ilala imesema kuwa maafisa biashara katika Manispaa hiyo kuhakikisha hawaruhusu watu kufanya biashara ya kemikali, bila kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa serikali (GCLA).
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Halmshauri ya Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri wakati akifunga mafunzo kwa Maafisa Biashara wa Manispaa hiyo ,jijini Dar es Salaam.
Amesema Kemikali kuwa wafanyabiashara wanaohitaji leseni wanatakiwa kuwa na kibali cha GCLA.
Shauri amesema mafunzo hayo ni mafunzo maalum kwa maafisa biashara kuwa uwezo kudhibiti kemikali zinazoingia katika njia zisizo sahihi na kuleta madhara kwa wananchi na kusababisha serikali kutumia fedha nyingi kutatua tatizo la kemikali.
Amesema zipo aina mbalimbali za dawa ambazo zimepigwa marufuku kutokana na athari zake kwa wananchi hivyo watu wakipata leseni lazima wafuatiliwe zaidi kwa kushirikiana na GCLA.
"Msipopata kibali kutoka GCLA kuhusiana na kemikali kutumika, ni vyema maafisa biashara msitoe leseni “amesema Shauri
Shauri aliwataka maafisa hao kuhakikisha leseni wanazotoa kwa wafanyabiashara, ziwe na lengo la kulinda afya ya walaji na mazingira kwa mustakabali wa kizazi cha sasa na cha baadae.
Akizungumza katika mafunzo hayo Mkemia Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya (DCEA) Ziliwa Machibya alisema, umakini mkubwa unahitajika katika kudhibiti kemikali kwani nchi nyingi zimepata matatizo ya kemikali kutokana na kukosa udhibiti
“Wafanyabiashara kwa wakati mwingine, hutumia kemikali ambazo hazijadhibitiwa kutengeneza dawa za kulevya au kemikali zilizopigwa marufuku.
“Potassium permanganate inatumika kusafishia maji lakini ikitumika vibaya watu hutengenezea Kokeini hivyo kemikali hizi bashirifu (zilizoruhusiwa) kutokana na kwamba haziepukiki lazima kudhibiti ili kuepusha uchepushaji”alisema.
Machibya alisema miongoni mwa changamoto zilizopo sasa katika udhibiti wa kemikali, ni kuongezeka kwa wataalam katika maabara za siri na usiri katika maabara juu ya utengenezaji wa kemikali hizo,
Meneja wa Kanda ya Mashariki Dunstan Mkapa wa GCLA amesema mafunzo hayo ni kutaka maafisa biashara kuwa na ukaribu na GCLA wakati wanatoa leseni kuwa na kibali kutoka katika mamlaka hiyo.
Kwa upande wake Mkaguzi wa kemikali GCLA Emanuel Lewanga alisema katikka kudhibiti athari za kemikali katika jamii kampuni ndani za halmashauri zinazohusika kukusanya kemikali taka kwaajili ya uteketezaji wanapaswa kujisajili.
Hiyo ni kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa matumizi ya kemikali majumbani na viwandani namba 3 ya mwaka 2013 sura ya 182 .
“Tumewaelekeza maafisa biashara ambao ndio watu wa msingi sana kwamba mtu anayetaka kujishughulisha na biashara ya kemikali lazima asajiliwe GCLA ikiwemo na wale wanaokusanya taka zitokanazo na kemikali”alisema.
Amesema athari ambazo zinaweza kutokea endapo mtu hakusajiliwa kujihusisha na masuala ya kemikali, ni uteketezaji unaoweza kuleta athari kwa wananchi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri akizungumza wakati wa kufunga mafunzo kwa maafisa biashara wa manispaa hiyo kuhusiana na utoaji wa leseni kwa wafanyabiashara wa Kemikali iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA)
Mkaguzi wa Kemikali wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Emanuel Lewanga akitoa mada ya kemikali kwa maafisa biashara wa Manispaa ya Ilala katika mafunzo yaliyoandaliwa na GCLA jijini Dar es Salaam.
Mkemia Mwandamizi wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya (DCEA) Kiliwa Machibya akitoa mada ya Kemikali Bashirifu katika mafunzo ya maafisa biashara wa Manispaa ya Ilala.
Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) Dunstan Mkapa akitoa maelezo kuhusiana na mkakati wa utoaji wa mafunzo ya Kemikali kwa maafisa biashara.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri akiwa katika picha ya pamoja na maafisa biashara wa manispaa hiyo na Watendaji wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia mkuu wa serikali GCLA mara baada ya kufunga mafunzo.
No comments:
Post a Comment