Na Abdullatif Yunus Michuzi Tv.
Benki ya CRDB imeendelea kutoa Semina Wezeshi kwa Mawakala wake Mkoani Kagera Juu ya namna ya kuboresha huduma zitolewazo na Benki hiyo kitengo Cha Mawakala, katika Ukumbi wa E.L.C.T Bukoba Agosti 19,2020.
Semina hiyo iliyozinduliwa na Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti, imehudhuliwa na Mawakala zaidi ya 100 kutoka katika Matawi ya Wilaya za Bukoba mjini, Muleba & Rwamishenye ikiwa ni muendelezo wa semina hizo kwa kanda ya ziwa na maeneo mengine ya Nchini.
Tangu kuanzishwa kwa huduma ya Mawakala mnamo Mwaka 2013, kwa sasa CRDB ina mawakala zaidi ya 16,000 waliotapakaa Tanzania nzima, na ina mawakala zaidi ya 400 katika Mkoa wa Kagera, hii inafanya CRDB kuwa na mawakala wengi kuliko Benki yeyote Nchini ikiwa imetengeneza takribani zaidi ya ajira elfu 20.
Mawakala wa CRDB wamesaidia kuongeza huduma za kibenki kwa kuongeza muda wa wateja kufanya miamala ambapo baadhi ya mawakala wanatoa huduma kwa masaa 24.
Semina ya mawakala imelenga pia kuwakumbusha mawakala kufuata taratibu na kanuni zote za kifedha kama zinavyosimamiwa na Benki kuu. Wakala hao wamepewa Elimu kuhusiana na elimu ya utakatishaji Fedha. Sambamba na Hilo CRDB imetoa elimu ya ujasiliamali na njia nzuri zaidi ya kuhudumia wateja wa benki, pamoja na kusaidia kuongeza wateja ili wananchi waendelee kufurahia huduma zetu, pia CRDB wamewakumbusha huku mawakala hao wakikumbushwa Juu ya kuhudumia wateja wao kwa uadilifu mkubwa na kuhakikisha wanatunza siri za wateja kwa uaminifu mkubwa
Meneja wa CRDB Tawi la Bukoba, Synden Bakari akizungumza kabla kumkaribisha Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti kuzungumza na Mawakala wa Mkoa Kagera.
Meneja wa CRDB Tawi la Mulebba, Mr. Mbaga akisistiza na kutolea ufafanuzi Jambo wakati wa maswali na majibu ndani ya Ukumbi wa ELCT Bukoba.
No comments:
Post a Comment