A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, July 27, 2020

RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA KUAGWA KESHO KITAIFA UWANJA WA UHURU, SERIKALI YATANGAZA UTARATIBU ULIVYOWEKWA

*Mawaziri,Makatibu wakuu,  wakuu wa idara, mabalozi, viongozi wa kisiasa,viongozi wa dini kuondokea Karimjee


Na Said Mwishehe,Michuzi TV

SERIKALI imetangaza utaratibu ambao utatumika kesho Jumanne ambayo ni siku ya kitaifa kuaga mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Katika utaratibu huo viongozi wa ngazi mbalimbali  hawataruhusiwa kwenda na  magari yao Uwanja wa Uhuru na badala yake kutakuwa na magari yatakaoanzia Karimjee jijini Dar es Salaaa.Usafiri utakuwepo kuanzia saa 12:30 asubuhi na gari ya mwisho itaondoka saa 1:30 asubuhi ya hiyo kesho.

Akitangaza leo Julai 27,2020, utaratibu mzima utakavyokuwa kwa siku ya kesho Jumanne, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Hassan Abbas ambaye ni Msemaji Mkuu wa Serikali kwamba ratiba ya kesho itakuwa ndefu.

"Leo shughuli za kuaga zimeendelea tangu asubuhi kwa viongozi mbalimbali kwa mana mawaziri,makatibu wakuu,wakuu wa idara,maofisa wengine wa utumishi na sekta binafsi walikuwa wakiaga  na baad ya kumaliza wananchi wakaendelea,"amesema Dk.Abbas.

Kuhusu kesho amesema shughuli zitaanza kwa Misa itakayoanzaa saa moja asubuhi hadi saa tatu asubuhi katika Kanisa la St.Imaculate jijini Dar es Salaam na baada ya hapo mwili wa mpendwa wetu Rais mstaafu Benjamin Mkapa utapelekwa Uwanja wa Uhuru ambako shughuli zote za kuaga kitaifa zitafanyika.

"Tunaomba wananchi wafike uwanjani mapema na kishaa kwa kukaa kwa utaratibu mzuri uliowekwa,"amesema Dk.Abbas na kuongeza ni vema wanaokwenda uwanjani wakawahi mapema.

Kuhusu viongozi ambao wanakwenda katika shughuli hiyo ya kitaifa ni kwamba wanaombwa magari yao wakaache Karimjee ambapo katika viongozi wamo mawaziri,makatibu wakuu,wakuu wa idara,mabalozi, viongozi wa dini,wawakilishi wa vyama vya kisiasa na viongozi wengine kutoka maeneo mbalimbali.

"Utaratibu amber utatumika kutakuwa na usafiri pale Karimjee na hivyo viongozi wote , mabalozi, na makundi mengine yote ya aina hiyo watatakiwa kufika mapema Karimjee na kisha kutakuwa na magari maalum yatakayokuwa yanawapeleka Uwanja wa Uhuru.Hivyo wasitumie.magari yao kuwapeleka uwanjani,"amesema Dk.Abbas.

Wakati huo huo amesema jambo jingine kwa hiyo kesho, baada ya kumalizika kwa ratiba ya kuaga mwili wa mzee wetu utakwenda kijijini Lupaso mkoani Mtwara hiyo hiyo kesho.

Amefafanua kuwa baada ya kufika huko siku ya Jumatano shughuli zitaanza kwa Misa saa mbili asubuhi na zitaendelea hadi muda wa kuupumzisha mwili wa Rais mstaafu, mzee Mkapa.

Akizungumzia zaidi shughuli hizo, Dk.Abbas amefafanua pamoja na mambo mengine , salamu za rambirambi zimeendelea kutolewa na viongozi wa mataifa mbalimbali  na kesho zitasomwa vizuri licha ya baadhi ya viongozi kuweka salamu zao kwenye mitandao ya kijamii."Viongozi wa ngazi mbalimbali kesho watashiriki shughuli hizi za kumuaga mpendwa wetu."

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages