A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, June 20, 2020

WILAYA YA UBUNGO YAKAGUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO YAWAJENGEA MACHINGA SOKO LA MILIONI 480

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic akitoa maelezo kwa viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya Hiyo Mhe.Kisare Makori pamoja na Mwenyekiti wa CCM  wa wilaya hiyo Lucas Mgonja na wengine wengi wakati walipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ikiwemo   majengo yanayojengwa soko kwaajili ya wafanya biashara ndogondogo (machinga), ambapo ujenzi huo utakapo kamilika utagharimu kiasi cha shilingi milioni 480 za kitanzania.
Mkuu wa Wilaya Wilaya ya Ubungo Mhe.Kisare Makori (katikati), akizungumza na Viongozi mbalimbali kutoka Chama Tawala cha CCM wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali katika wilaya hiyo.
Mwenyekiti wa CCM  Wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja akizungumza wakati wa ziara hiyo

Mmoja ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM  Wilaya ya Ubungo akichomea wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa wilayani humo kukagua mradi wa ujenzi wa soko la kisasa la wafanya biashara  ambapo ujenzi huo utakaotumia shilingi milioni 480 za kitanzania 
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic (kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mradi wa Ujenzi wa Soko la wafanya biashara ndogondogo, Nuru Liyau, ambapo ujenzi huo utakapo kamilika utagharimu kiasi cha shilingi milioni 480 za kitanzania 
Muonekano wa Soko hilo 
Baadhi ya viongozi na wanakamati wa siasa wilaya ya ubungo wakiwa katika ziara hiyo
Mkuu wa Wilaya Wilaya ya Ubungo Mhe.Kisare Makori akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja  wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali. Picha zote na Brian Peter


MATUKIO KATIKA PICHA
 
 


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages