A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, June 2, 2020

TPA YAIPIGA JEKI SERIKALI SEKTA YA AFYA YAKABIDHI VIFAA VYA UJENZI NA TIBA KWA RC MAKONDA.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, akipokea msaada Vifaa vya ujenzi pamoja na Vifaa tiba kutoka kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Augustino Wittonde, kwaajili yakusaidia serikali upande wa sekta ya afya hafla ya makabidhiano hayo imefanyika katika viwanja vya JKT Mgulani jijini Dar es Salaam.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Augustino Wittonde, akizungumza wakati wa hafla yakukabidhi  msaada wa Vifaa vya ujenzi pamoja na Vifaa tiba vikiwa na thamani zaidi ya shilingi milioni 120 walivyokabidhi kwa Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kwaajili ya kuipiga jeki serikali ya mkoa upande wa sekta ya afya.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda wakati wakupokea msaada huo.

RC Makonda amesema wanaendelea na ujenzi wa ofisi za Walimu na kuboresha huduma za afya kwa kutoa vifaa na wahudumu wa kutosha katika hospitali ambazo zimejengwa kwa maelekezo ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Pone Magufuli.

Amezungumza hayo wakati wa hafla ya kupokea vifaa tiba na ujenzi vilivyo tolewa na Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA. Pia RC Makonda amesema anaishikuru Mamlaka ya Bandari kwa kumvisha nguo wiki mbili zilizopita alitoa ahadi ya mashine mbili za Utrasound Katika hospitali Mpya iliyoko Wilayaya Kigamboni  hivyo kwa msaada uliyotolewa na TPA utasaidia kwa hospitali hiyo kuanza kazi mara moja.

Upande wake Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Augustino Witonde amesema kuwa wataendelea kutoa misaada mbalimbali ili kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za serikali.

Witonde arsenal tumetoa mashine mbili za Utrasound kubwa na ndogo pia milango ya alminium 37 na madirisha 27, milango ya magril 8 na madirisha 53 vyote hivyo vimetengenezwa na Jeshi la Kujenga Taifa JKT.

Hata hivyo Mhandisi Witonde amesema vifaa vyote hivyo vinagharimu takribani shilingi Milioni 120 na kuwataka wananchi waendelee kutumia Bandari yao na rasilimali zake.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh Felix Lyaviva amesema TPA wamekuwa wakitoa misaada mbalmbali kuunga mkono juhudi za serikali na hawapo mbali na Wilaya yake kwakuwa mwaka jana walitoa mashuka na round Table kwaajili ya kujifungulia wakina mama leo tena wameamua kukabidhi vifaa hivi tena muhimu sana hasa kwa kipindi hiki cha mfumuko wa janga la Corona na omba tuvipokee kwa mikono miwili.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages