Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza wakati wa Kikao na Vijana wa UVCCM Mkoa wa Dar es salaam,
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza wakati wa Kikao na Vijana wa UVCCM Mkoa wa Dar es salaam alipoalikwa na mwenyekiti wa vijana mkoa..
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda pamoja na Mkuu waMkoa wa Arusha Mrisho Gambo pamoja na viongozi wenine wakiserebuka nyimbo maalum baada yakumalizika kwa mkutano huo
Baadhi ya wanachama wa CCM wakiserebuka wakati wa mkutano huo Picha zote na Brian Peter
Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam Mhe. Paul Makonda amewataka Vijana wa Chama cha Mapinduzi kukilinda
Chama hicho na kuwa mabalozi wazuri wa kuyaeleza maendeleo
yaliyofanywa na Rais
Dkt. John Maguguli katika kipindi cha Miaka Mitano.
RC Makonda ametoa
kauli hiyo wakati wa Kikao na Vijana wa UVCCM Mkoa wa Dar es salaam ambapo
amesema yapo Maendeleo Makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano na
kama wasipoyazungumzia watatoa mwanya kwa watu wasiolitakia mema Taifa
kupenyeza Wongo.
Aidha RC Makonda
amewataka Vijana hao kuwa macho hususani kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi
Mkuu kwakuwa wapo baadhi ya watu wenye tamaa watakuwa tayari kuvunja hata Amani
ili tu wapate fedha za kushibisha matumbo yao.
Pamoja na hayo RC
Makonda amesema ifikapo Juni 20 ataanza ziara na Kamati ya Siasa ya Mkoa kwa
lengo la kukabidhi kwa Chama miradi yote iliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya
Tano chini ya Uongozi imara wa Rais Magufuli.
Hata hivyo RC Makonda
ametoa Msaada wa Mabati na Mbao za kupaua kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa
Ofisi ya UVCCM Wilaya ya Kigamboni.
MATUKIO KATIKA PICHA
No comments:
Post a Comment