Mamia ya watu wamefanya maandamano jana usiku kwenye mitaa ya Hong Kong ikiwa ni kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kuanza kwa maandamano ya kuipinga serikali, huku kiongozi wa mji huo Carrie Lam akitoa wito wa amani na utulivu.
Aliwaambia wanahabari kuwa kila mmoja lazima ajifunze ikiwemo serikali ya Hong Kong akiongeza kuwa mji huo hauwezi kuvumilia aina hiyo ya vurugu, na watu wa Hong Kong wanataka mazingira ya amani na utulivu ili waishi na kufanya kazi kwa furaha.
Maandamano ya jana yalifanyika licha ya onyo kutoka kwa polisi kuwa washiriki wangekabiliwa na nguvu na kupewa adhabu ya hadi miaka mitano jela. Karibu watu 25 walikamatwa kwa kushiriki katika maandamano hayo ambayo hayakuruhusiwa.
Miezi saba ya maandamano makubwa yenye ghasia yalianza Juni 9 mwaka jana wakati zaidi ya watu milioni moja walipoingia mitaani kupinga mswada wa sheria inayoruhusu watu kupelekwa China bara wanapofanya makosa.
No comments:
Post a Comment