Taarifa ya makao rasmi ya Malkia kutoka kasri la Buckingham imesema utofauti katika sherehe hizo kwa mwaka 2020 unatokana na kuzingatia kanuni za kujitenga zilizotangazwa na serikali kuzuia kusambaa virusi vya corona.
Malkia Elizabeth na mumewe Philip waliondoka mjini London na kwenda katika kasri la Windsor mapema mwezi April kama sehemu ya tahadhari ya janga la virusi vya corona na leo ilikuwa mara ya kwanza kuonekana hadharani tangu wakati huo.
Malkia Elizabeth wa II ambaye alizaliwa mwaka 1926 ameitawala Uingereza tangu mwaka 1952 alipochukua hatamu za falme hiyo akiwa na umri wa miaka 25
No comments:
Post a Comment