Katika uchunguzi wa awali wa Polisi uliofanyika baada ya kutokea ajali hiyo imebainisha kwamba chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa daladala kushindwa kufuata Sheria za usalama barabarani jambo ambalo linagharimu maisha ya watu na mali.
Jeshi la Polisi kikosi cha TAZARA linaendelea kumtafuta dereva wa Gari hilo ambaye alikimbia baada kutokea ajali hiyo ili sheria ichukue mkondo wake. Majeruhi walikimbizwa hospitali ya Pugu Kajiungeni kwa matibabu na hali zao kwa mujibu wa taarifa za daktari wanaendelea vizuri.
Mwili wa marehemu ulipelekwa hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi.
Niendelee kutoa wito kwa wananchi ikiwemo vyombo vyote vya moto kama magari kuheshimu sheria za usalama barabarani kwani katika vivuko vya reli zipo alama ambazo kama dereva ama mtembea kwa miguu anatakiwa kuzifuata kabla ya kuvuka.
Aidha, katika maeneo yote yanayopitiwa na miundombinu ya reli ya TAZARA wananchi waendelee kuthamini na kulinda miundombinu hiyo kwani ni faida kwao kama chanzo cha mapato na Uchumi wa nchi kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment