A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, June 13, 2020

HUKUMU 12 ZAUHUJUMU UCHUMI ZATOLEWA SIMIYU KIPINDICHA MWAKA HUU


Jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu na Mahakama ya Wilaya ya Bariadi.
Sehemu ya kumpunzika ya wananchi  kwa ajili ya kupatia huduma za Mahakama.
Hakimu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu Mhe. Venance  Mlingi, akizungumzia kuhusu usikilizaji wa mashauri baada ya uboreshaji wa miundombinu ya Mahakama.
Mtendaji wa Mahakama ya Mkoa wa Simiyu, Bw. Leonard Maufi alisema uboreshaji wa miundombinu, ulivyosaidia utendaji kazi katika huduma za utoaji haki kwenye Mahakama hiyo.
Msaidizi wa Kumbukumbu Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu, Bw. William Mbeke akizungumza kuhusu utunzaji wa nyaraka na kumbukumbu za Mahakama katika Mahakama hiyo.
********************************


Na Innocent kansha na Magreth Kinabo – Mahakama,Simiyu

Jumla ya mashauri 28 ya uhujumu uchumi yamefunguliwa na hukumu 12 zimetolewa kutokana na makosa ya aina hiyo zimefunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Simiyu pamoja na Mahakama ya Wilaya Bariadi.

Akifafanua chanzo cha makosa hayo kwa Maafisa Habari wa Mahakama ya Tanzania, ofisini kwake katika mahojiano maalum, Hakimu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu Mhe. Venance Mlingi alisema yanatokana na wananchi kuingia kwenye Hifadhi za Taifa za Wanyama Pori ya Serengeti na Pori la akiba Maswa.

“Mashauri mengine tunayoyapokea ni ya madawa ya kulevya , bangi na mirungi alikadhalika mashauri ya talaka na mirathi, lakini mashauri mengi tunayoyapokea kwa wingi zaidi ni ya kuingia hifadhini na kukutwa na nyara za Serikali na silaha kama vile, kisu, panga na rungu ,’’ alisema Mlingi.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Hakimu huyo zinaonyesha kuwa Desemba mwaka 2019, Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya Bariadi zilibakiwa na mashauri ya uhujumu uchumu yapatayo 125 yalibaki kwa sababu mbalimbali ikiwemo kutokamilika kwa upelelezi na mengine kukosa kibali cha kuyasikiliza kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP).

Mlingi alifafanua kwamba kuanzia Januari mwaka 2020 hadi Juni Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya Bariadi zilifanikiwa kusajili mashauri ya uhujumu uchumi yapatayo 28 na kumaliza mashauri 51,na kubakiwa na mashauri yapatayo 102.

Aliongeza kuwa kutoka na mashauri ya uhujumu uchumi Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya ya Bariadi zilifanikiwa kutoa hukumu 12 za vifungo jela kwa watuhumiwa waliothibitika kutenda makosa hayo visivyopungua kuanzia miaka 20 hadi 30 jela.

Mlingi alizungumzia pia kuhusu hali ya usikilizaji wa mashauri kwa upande wa Mahakama za Mwanzo katika Mkoa wa Simiyu wamefanikiwa kumaliza mashauri yote ndani ya miezi sita ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya viongozi wa Mahakama kwa asilimia 100, licha ya kujiwekea malengo ya kumaliza mashauri yote ndani ya miezi mitatu kila Hakimu, hivyo huwa amemaliza mashauri yake katika na hilo limefanikiwa.

Aliongeza kwamba katika Mahakama hiyo, wanatoa elimu kuhusu masuala ya kisheria yanayohusu mirathi, ndoa na migogoro ya ardhi kwa wananchi ili kuwapa uelewa.

‘‘Ninaomba wananchi wafike katika Mahakama hii, ili kuweza kapata elimu yya masuala mbalimbali ya kisheria, hili ni jengo lao kwa ajili ya kupata elimu pia, alisisitiza Mlingi.

Alisema kwa mwaka Mahakama ya Hakimu Mkazi mashauri yanayofunguliwa ni wastani mashauri 120 na Mahakama ya Wilaya ya Bariadi ni 660.

Kwa upande wake Mtendaji wa Mahakama ya Mkoa wa Simiyu, Bw. Leonard Maufi alisema uboreshaji wa miundombinu ya Mahakama imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama kubwa za ulipaji wa pango kwani ikubukwe kuwa awali Mahakama ya Mkoa wa Simiyu ilikuwa inatumia jengo la mtu binafsi kuendeshea shughuli zake za utoaji haki.

Hivyo ghrama za ulipaji kodi katika jengo hilo zilikuwa ni kubwa, na lilikuwa haikidhi hadhi ya Mahakama na walikuwa wanatumia kiasi cha shilingi milioni 3 kila mwezi kwa ajili ya malipo ya pango hilo, lakini kwa sasa fedha hizo zinaelekezwa kwenye matumizi mengine ya shughuli za Mahakama.

“ Kutokana na maboresho haya ari ya watumishi ya utendaji kazi ipo juu sana na ufanisi wa kazi umeongezeka kwa kiwango kikubwa na kila mtumishi anafanya kazi kwa nafsi, vifaa na vitendea kazi vipo vya kutosha,’’.

Maufi alisema hali hiyo imeongeza ubora wa utoaji huduma kwa wadau wa Mahakama, utunzaji wa nyaraka na kumbukumbu za mahakama umeboreka .

Baadhi ya wananchi waliofika mahakamani hapo walisema wameridhika na huduma zinazotolewa na kushukuru Serikali kujenga jengo hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages