A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, May 28, 2020

TAKUKURU Yaanika Lilipofikia Jarada la Kangi Lugola

 
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) imeeleza lilipofikia Jarada la tuhuma za aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola na wenzanke ambao kwa pamoja wanatuhumiwa kusaini mkataba wa zaidi ya Tsh trilioni 1 na kampuni ya ROMANIA kununua vifaa vya zimamoto kinyume cha taratibu.

Hayo yamesemwa Alhamisi, Mei 28, 2020 na Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma wa TAKUKURU, Joseph Mwaiselo wakati akifanya mahojiano na +255 Global Radio.

Januari 23, 2020 Rais wa Tanzania, John Magufuli alitangaza kutengua uteuzi wa Lugola na Andengenye huku akiridhia barua ya kujizulu ya Meja Jenerali Kingu na kuagiza Takukuru kuanza uchunguzi kwa wote waliohusika bila kujali nafasi zao.

“Hii tuhuma ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (Kangi Lugola) na Kamishna General wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, sisi Takukuru tulishakamilisha kazi yetu na suala hili lipo kwenye ofisi ya DPP nadhani yeye ndiye anayeweza kuwa msemaji katika hili kwa sasa.

“Hakuna upendeleo katika kushughulikia rushwa, utendaji wetu wa kazi unaongozwa kwa mujibu wa sheria, inapotokea jalada fulani limechelewa ni kutokana na mfumo wa ushahidi. Utaratibu wa kuzirudisha zile fedha zilizopatikana kwa njia ya ubadhirifu upo kwa mujibu wa sheria, zinarudishwa serikalini na ndio msimamo wa dunia.

Januari 23, 2020 Rais wa Tanzania, John Magufuli alitangaza kutengua uteuzi wa Lugola na Andengenye huku akiridhia barua ya kujizulu ya Meja Jenerali Kingu na kuagiza Takukuru kuanza uchunguzi kwa wote waliohusika bila kujali nafasi zao.

Kuhusu uchaguzi mkuu.
“Uchaguzi ni fursa, sisi kama wananchi tunatakiwa kukaa na kuanisha changamoto zetu ambazo tumekutana nazo kwa takriban miaka mitano. Katika nchi 35 za bara la Afrika, Tanzania imeongoza kwa kudhibiti rushwa kuanzia mwaka 2015.

Rushwa ya ngono.
Rushwa ya ngono inaondoa utu, inasababisha aibu. “Hata kama amesikia kwa mtu atuambie amepewa taarifa na nani ili iwe rahisi kushughulikia.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages