A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, May 19, 2020

MO DEWJI FOUNDATION WAKISHIRIKIANA NA KLABU YA SIMBA WAHITIMISHA ZOEZI LA UGAWAJI WA BARAKOA.


20200518_130454

20200518_130459

20200518_130502

20200518_131641

Na Zainab Nyamka, Dar es Salaam

Klabu ya Simba kwa kushirikiana na Taasisi ya Mo Dewji  imehitimisha zoezi la ugawaji wa Barakoa kwa wakazi wa maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam.

Zoezi hilo limehitimishwa kwa watendaji wa taasisi hiyo kukabidhi barakoa kwa ajili ya kujilinda na homa kali ya Mapafu (COVID-19) inayosababishwa na virusi vya corona.

Ikiwa ni siku ya tatu toka kuanza kwa ugawaji wa barakoa hizo, wananchi wamefurahia zoezi hilo la kuwakumbuka wananchi hususani wale ambao hawana uwezo wa kununua wenye kipato cha chini.

Barakoa zimekuwa zikishauriwa kutumiwa kama njia ya kupunguza uwezekano wa kusambaza virusi hivo pale ambapo mtu atakua ana kohoa ama kupiga chafya pamoja na kupunguza umbali ambao maji maji hayo yanaweza kuruka.

Barakoa hizo zimetengenezwa hapa nchini na kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited kwa kutumia pamba inayolimwa hapa nchini. Barakoa hizi ni imara na hivo kuruhusu uwezekano wa kutumika zaidi ya mara moja baada ya kufuliwa na kupigwa pasi.

Klabu ya Simba imeendelea kuchukua tahadhari kwa kuwalinda wachezaji wake na zoezi hili limekua na lengo la kuwakumbuka wananchi na mashabiki wake pamoja na kuwasihi waendelee kufuata hatua zinazoelekezwa.

Taasisi ya Mo Dewji  imejitolea barakoa 25,000 kwa Mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wa kurudisha kwa jamii kwa kuangalia namna bora ambazo inaweza kusaidia katika mapambano dhidi virusi vya corona. Hususani kwa wananchi wa kawaida kuweza kujilinda na kupambana na virusi hivo.

Ugawaji wa barakoa hizo umefanyika katika masoko na vituo vya boda boda mbali mbali jijini Dar es Salaam ikiwemo maeneo ya Kivukoni, Kariakooo, Tandale, Manzese, Buguruni, Makumbusho, Mabibo, Temeke, Mbagala, Msasani, Kimara, Mbezi na Tegeta

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages