A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, May 21, 2020

RC MAKONDA ATANGAZA PUNGUZO LA BEI HADI 80% KWENYE MADUKA YA NGUO DAR WATU WAFURAHIE KUPUNGUA KWA CORONA.

Paul-Makonda

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametangaza Punguzo kubwa la Bei ya Nguo la hadi 80% kwenye Maduka Makubwa ya Nguo yaliyopo Jijini humo ili kuhakikisha Wananchi wanapendeza na kuwa nadhifu Jumapili ya May 24 kwenye Kilele cha Siku Tatu za Shukrani Kwa Mungu zilizotangazwa na Rais Dkt. John Magufuli.

RC Makonda amesema Miongoni mwa Maduka Makubwa yaliyoamua kutoa punguzo la bei ni pamoja na Mr. Price na Red Tag ya Mlimani city, Vunja Bei, Maduka yaliyopo City Mall pamoja na Maduka Mengine yaliyopo Posta, Kariakoo, Kinondoni na Sinza.

Aidha RC Makonda amesema atafurahi kuona kila mwananchi wa mkoa huo anasheherekea kwa nderemo na vifijo siku ya jumapili kama sehemu ya shukrani kwa Mungu kwa kutukinga na Corona na baada ya hapo kila mmoja achape kazi ili kwa pamoja tuinue Uchumi wa Taifa.

Pamoja na hayo RC Makonda ametangaza Shindano la DJ bora ambapo kila DJ atatakiwa kumtumia Video Clip huku akiwaelekeza wenye Bar, Hotel, Lodge, Band na Biashara kuzifungua.

Kwa Upande wao wamiliki wa Maduka ya Mr. Price, Red Tag na Maduka Mengine wamewakaribisha Wananchi kujitokeza kwa wingi kufanya manunuzi huku wakimpongeza RC Makonda kwa kuwapigania Wananchi wa mkoa huo ili kuhakikisha wanapata mavazi mazuri kwa bei nafuu

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages