A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, May 30, 2020

RAIS MAGUFULI AWAKABIDHI MARAIS WASTAAFU TAUSI 25 KILA MMJO NA MAMA MARIA NYERERE KWAKUTAMBUA MCHANGO WAO KATIKA TAIFA.

1.-4-962x1024
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Hati ya Makabidhiano ya zawadi ya Ndege aina ya Tausi 25 kwa Mama Maria Nyerere mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya kuwafuga katika Makazi yake, hafla hiyo fupi ilifanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma.
2-24-1024x858
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi hati ya Makabidhiano ya ndege aina ya Tausi 25 kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi kwa ajili ya kuwafuga katika makazi yake. Hafla ya Makabidhiano hayo imefanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
3AAA-1024x962
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi hati ya Makabidhiano ya ndege aina ya Tausi 25 kwa Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa kwa ajili ya kuwafuga katika makazi yake. Hafla ya Makabidhiano hayo imefanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
4AAA-2-1024x951
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi hati ya Makabidhiano ya ndege aina ya Tausi 25 kwa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete kwa ajili ya kuwafuga katika makazi yake. Hafla ya Makabidhiano hayo imefanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
5AA-2-1024x606
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi hao Wakuu wastaafu mara baada ya kuwakabidhi zawadi ya ndege aina ya Tausi.
6AAA-1-1024x812
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika hafla hiyo fupi ya Makabidhiano ya zawadi ya ndege aina ya Tausi.
7AAA-1-1024x713
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete wakati akitoa neno la Shukrani kwa niaba ya Marais wenzake wastaafu.
8AAA-1-1024x819
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete mara baada ya hafla fupi ya Makabidhiano ya ndege aina ya Tausi katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
9AAA-1-1024x682
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages