A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, May 28, 2020

MBUNGE WA KAWE ANAKESI YA KUJIBU-MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU

Na Karama Kenyunko Michuzi TV 
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema Mbunge wa Kawe, Halima Mdee anayekabiliwa na kesi ya uchochezi kwa kutoa maneno ya kuudhi dhidi ya Rais John Magufuli anayo kesi ya kujibu.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ametoa uamuzi huo leo Mei 28, 2010 wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutolewa uamuzi.

Hatua hiyo imekuja baada ya Februari 20, mwaka huu upande wa mashtaka kufunga ushahidi wao kufuatia mashahidi watatu waliofika mahakamani hapo kutoa ushahidi ambao leo mshtakiwa Mdee ameonekana na kesi ya kujibu.

Hata hivyo Mdee kupitia wakili wake Hekima Mwasipo amesema mteja wake atajitetea kwa kiapo na atakuwa na mashahidi watano.

Katika kesi hiyo, inadaiwa kuwa Julai 3,2017 katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iliyopo mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni, Mdee anadaiwa kutamka maneno dhidi ya  Rais John Magufuli kuwa  “anaongea hovyohovyo , anatakiwa  afungwe breki”  na kwamba kitendo ambacho kingeweza  kusababisha uvunjifu wa amani.  

Mdee alifikishwa mahakamani hapo Julai 10, 2017 na yupo nje kwa dhamana.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages