A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, May 16, 2020

KENYA YAFUNGA MPAKA WA TANZANIA NA SOMALIA NA KUONGEZA SIKU 21 ZA WATU KUKAA NDANI.


Kenya imefunga kwa muda wa siku 30 mipaka yake ya kimataifa ya Tanzania na Somalia kuanzia saa sita usiku wa Jumamosi Mei 16,2020.

Katika hotuba yake kwa taifa Rais Uhuru Kenyatta amesema hatua hiyo inajumuisha udhibiti usafiri wa watu kutoka mataifa hayo kuingia nchini Kenya.

Hata hivyo usafirishaji wa mizigo utaendelea kati ya Kenya na mataifa hayo mawili.

Marufuku hiyo ya kuzuia watu kutoka Tanzania na kuingia nchini Kenya inaanza usiku wa leo saa 6 na kuruhusu mizigo tu kupita. Na kwa upande wa Somalia masharti ni hayo hayo, mizigo peke yake ndio itaruhusiwa.

“Katika wiki moja iliyopita Maambukizi ya Watu 43 hapa Kenya yalikuwa ni kutoka nje ya Nchi, hii inaleta wasiwasi, tumeamua sasa kuanzia saa sita usiku wa leo tunafunga mipaka yetu ya Kenya-Tanzania na Kenya-Somalia, watakaoruhusiwa kuingia ni Madereva wa mizigo pekee”

Aidha madereva watakaoingia nchini Kenya kupeleka mizigo watatakiwa kupima corona kwanza huku ikimeongeza tena muda wa marufuku ya kutoka nje kwa muda wa siku 21.

Kufikia sasa idadi ya watu walioambukizwa  virusi vya corona nchini Kenya imeongezeka hadi 830 baada wagonjwa wapya 49 kuthibitishwa kuwa na ugonjwa huo.

Waliofariki kutokana na corona ni watu 50 baada ya wengine watano kufariki.

“Watu wengine watano wamefariki baada ya kuugua corona na kufanya idadi ya waliofariki na corona kufikia 50,  tuna wagonjwa wapya 49 pia na hii inafanya maambukizi ya corona kufikia 830 Kenya, wagonjwa 17 wamepona na kufanya waliopona kufikia 301”- Amesema Kenyatta

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages