Bunge la Umoja wa Ulaya linatarijiwa kukutana leo kwenye kikao maalum kujadiliana kuhusu msimamo wa pamoja katika kukabiliana na janga la virusi vya corona.
Wabunge hao wanatarajiwa kupigia kura azimio linalotaka raia wa Umoja wa Ulaya kulindwa kwa kiasi kikubwa katika kukabiliana na janga la ugonjwa wa COVID-19, umoja huo kusaidia mifumo ya afya ya nchi wanachama na mkakati sawa katika kuchukua hatua za dharura.
Rasimu ya azimio pia inaikosoa tabia ya nchi mbili wanachama, Hungary na Poland katika kukabiliana na mzozo wa virusi vya corona.
Wabunge wengi watahudhuria mkutano huo utakaofanyika kwa njia ya mtandao na wote watapiga kura kupitia barua pepe. Spika wa Bunge la Ulaya, David Sassoli atatangaza matokeo kesho.
No comments:
Post a Comment