Diwani wa
Kata ya Kimara Paschal Manota, akizungumza
na waandishi wa habari pamoja na wananchi wa kata hiyo kwa niaba ya Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa daraja
katika mto Gide uliopo kimara ambapo Daraja hilo litagharimu takribani Shilingi
za kitanzania milioni 321 ambapo katika hizo milioni 200 zimetoka kwenye mfuko
wa Halmashauri ya Ubungo na hizo nyengine zimetolewa na Wakala wa Barabara za Mijini
na VIjijini (TARURA)
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Ujenzi , Mpeha 2000 Ltd Never Black, akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wananchi wa
kata ya kimara wakati alipokabidhiwa eneo kwaajili ya Ujenzi wa daraja katika
mto Gide uliopo kimara ambapo Daraja hilo litagharimu takribani Shilingi za kitanzania
milioni 321 ambapo katika hizo milioni 200 zimetoka kwenye mfuko wa Halmashauri
ya Ubungo na hizo nyengine zimetolewa na Wakala za Barabara wa Mijini na VIjijini
(TARURA)
Msimamizi wa Mradi kutoka Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Manispaa
ya Ubungo Mhandisi Denis Charles akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wananchi wa
kata ya kimara wakati alipokabidhiwa eneo kwaajili ya Ujenzi wa daraja katika
mto Gide uliopo kimara ambapo Daraja hilo litagharimu takribani Shilingi za kitanzania
milioni 321 ambapo katika hizo milioni 200 zimetoka kwenye mfuko wa Halmashauri
ya Ubungo na hizo nyengine zimetolewa na Wakala za Barabara wa Mijini na VIjijini
(TARURA)
Mkazi wa kata
hiyo Mwajuma Mungila, akitoa neno la shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh John Magufuli pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda,
kwa kuwatatulia kero iliyodumu kwa muda mrefu zaidi ya miaka kumi.
Wanahabari wakiwajibika wakati wa hafla hiyo Picha zote na Brian Peter
Sasa Ujenzi wa daraja la mto
Gide kuanza kujengwa jumatatu baada ya wakazi wa kata hiyo kupata shida ya kutumia njia hiyo kwa muda wa miaka kumi
Akizungumza
na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam, Mkandarasi anaetarajia
kujenga daraja hilo Never black amezibitisha kuwa wanatarajia kuanza ujenzi huwo rasmi siku
ya Jumatatu Tarehe 30 mwezi huu.
“Tunatarajia
kuanza ujenzi haraka iwezekanavyo na tumepewa muda wa miezi mitatu yaani siku
90 lakini tunatarajia kufanya kazi kwa muda wa miezi miwili kama mvua itasimama
kunyesha au haitonyesha kwa wingi.
“Daraja litakuwa na
urefu wa mita kumi na moja na litakuwa la njia mbili ambalo lita ghalimu kiasi
cha shilingi za kitanzania milioni 321Daraja hilo litaweza kupitisha magari ya
uzito wa tani kumi pamoja na njia ya watembea kwa miguu” anasema Black.
Kwa upande wa Diwani wa
Kimara Baruti, Paschal Manota, anasema Halmashauri imetoa sh milioni 200, na
Wakala wa barabara, TARURA imetoa milioni 100 kwaajili ya mchango wa ujenzi wa
daraja hilo la mto Gide.
“Mkandarasi
anatakiwa atoe kazi kwa wananchi wa eneo la baruti na makoka asipewe mtu wa
kutoka mbali na eneo hili la ujenzi wa daraja ili lijenge kwa wakati.
No comments:
Post a Comment