Afrika inahitaji Dola Bilioni 100 ili kuboresha huduma za afya, kukabiliana na #Covid19
UN yasema huduma za afya ni dhaifu, #Covid19 itaharibu zaidi.
Aidha Umoja wa Mataifa umesema kwamba nchi nyingi za Afrika zimekuwa zikificha na kukataa kutoa taarifa sahihi za kasi ya maambukizi na vifo vitokanavyo na COVID-19.
Pia UN imebainisha kuwa Afrika inakabiliwa na uhaba mkubwa sana wa vifaa vya kupima virusi vya Corona na uhaba wa wataalamu wa kupambana na virusi hivyo achilia mbali uhaba wa vifaa tiba ikiwemo mashine za kupumulia, vifaa vya kujikinga n.k.
NOTE: Ikiwa unadhani wagonjwa 19 wa COVID-19 hapa Tanzania bado ni wachache na kwamba madhara ya Corona virus bado ni madogo sana nchini Tanzania utakuwa inajidanganya tu kuifurahia faraja isiyokuwepo.
Tazama takwimu za hali ya mambo ilivyokuwa kwa Mataifa ya wenzetu kisha chukua tahadhari. Hapa hatutishani ila tunaelezana hali halisi.
Italia
February 21,2020 - Wagonjwa 21
February 21,2020 - Wagonjwa 21
March 27,2020 - Wagonjwa 86,498
Marekani
February 21, 2020 - Wagonjwa16
February 21, 2020 - Wagonjwa16
March 27, 2020 - Wagonjwa 100,037
Ufaransa
February 26, 2020 - Wagonjwa 18
February 26, 2020 - Wagonjwa 18
March 27, 2020 - Wagonjwa 32,964
Ujerumani
February 25, 2020 - Wagonjwa 18
February 25, 2020 - Wagonjwa 18
March 27, 2020 - Wagonjwa 50,178
Hispania
February 27, 2020 - Wagonjwa 25
February 27, 2020 - Wagonjwa 25
March 27, 2020 - Wagonjwa 64,059
Iran
February 19, 2020 -Wagonjwa 5
February 19, 2020 -Wagonjwa 5
March 27, 2020 - Wagonjwa 32,332
Afrika Kusini
March 1, 2020 - Mgonjwa 1
March 27, 2020 - Wagonjwa 1,170
Nasisitiza tu hatutishani hapa ila ni vema Tanzania na Afrika kwa ujumla ikafahamu kuwa sio kwamba kwa sasa tupo vizuri, HAPANA, bali tupo pale wenzetu walipokuwepo wiki mbili tatu zilizopita.
Kama hatua madhubuti za kujikinga hazitachukuliwa nasi tutafika huko walipo wengine au huenda hata tukajipata taabani zaidi.
COVID-19 haichagui umri, rangi wala hali yako ya afya. COVID-19 inaua tena inaua haraka sana. Chukua tahadhari, chukua hatua!
Ni Wakati wa Kudumisha Umoja na Mshikamano wetu kwa kukumbushana juu ya Tahadhari za Ugonjwa Hatari wa CORONA #covid-19
Mimi Omary Ally Mgaza Kiongozi Wa UVCCM Wilaya ya Bagamoyo Naomba nikukumbushe ewe Ndugu, Jamaa na kila Mwanachi Kuzingatia hatua muhimu Katika kujikinga na Janga hili zito.
- Tuepuke kujumuika kwenye Mikusanyiko isiyo ya lazima
- Tusafishe Mikono yetu kila wakati
- Sio lazima tusalimiane kwa kupeana Mikono
Tujilinde ili Tuwalinde tuwapendao
No comments:
Post a Comment