A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, December 19, 2019

WORLDREMIT YAZINDUA HUDUMA YA GHARAMA NAFUU YA UTUMAJI WA PESA KWENDA AKAUNTI YA M-PESA NCHINI TANZANIA

Mkurugenzi wa WorldRemit ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Sharon Kinyanjui (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya WorldRemit itakayowawezesha wateja wa Vodacom M-Pesa kupokea pesa kutoka zaidi ya nchi 50 ulimwenguni. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni (katikati) na Meneja Maendeleo ya Biashara M-Pesa, Ruth Moshi (kulia).
Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya WorldRemit itakayowawezesha wateja wa Vodacom M-Pesa kupokea pesa kutoka zaidi ya nchi 50 ulimwenguni. Wengine ni Mkurugenzi wa World Remit ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Sharon Kinyanjui (katikati) na Meneja Mkazi wa World Remit Tanzania, Cynthia Ponera (kushoto).
Meneja Mkazi wa WorldRemit Tanzania, Cynthia Ponera (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya World Remit na Vodacom M-Pesa. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa World Remit ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Sharon Kinyanjui, Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni na Meneja Maendeleo ya Biashara M-Pesa, Ruth Moshi.

Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni (wapili kulia) akimkabidhi bango Mkurugenzi wa WorldRemit ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Sharon Kinyanjui kuashiria uzinduzi wa huduma ya WorldRemit itakayowawezesha wateja wa Vodacom M-Pesa kupokea pesa kutoka zaidi ya nchi 50 ulimwenguni. Wengine kushoto ni Meneja Mkazi wa WorldRemit Tanzania, Cynthia Ponera na Meneja Maendeleo ya Biashara M-Pesa, Ruth Moshi.
  • Wateja wa Vodacom M-Pesa kupokea pesa kutoka zaidi ya nchi 50 duniani kwa kutumia app ya WorldRemit kwa haraka
Desemba 17, 2019, Dar es salaam - Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na vinara wa kutoa huduma ya kutuma pesa kwa njia ya mtandao WorldRemit, watawawezesha zaidi ya watumiaji wa M-Pesa Zaidi ya milioni 10 kupokea pesa moja kwa moja katika akaunti zao kutoka kwa marafiki na familia wanaosafiri na kufanya kazi nje ya nchi.

Huduma hiyo mpya inaongeza urahisi wa wapokeaji wa uhamishaji wa pesa mijini na vijijini kwani wanaweza kupokea pesa kutoka kwa jamaa na marafiki nje ya nchi moja kwa moja kwenye simu zao, bila kuhitaji kuwa na akaunti ya benki au kuunganishwa katika mtandao.

WorldRemit ni mojawapo ya vinara ulimwenguni katika utoaji wa huduma ya uhamishaji pesa kupitia akaunti za simu ya mkononi, ambapo wameunganishwa na akaunti zaidi ya milioni 160 katika nchi 29. Mbali na huduma ya pesa kwa njia ya simu ya mkononi, kampuni hiyo pia inatoa huduma za uhamishaji wa kibenki, huduma ya kuchukua pesa papo hapo na kuongeza muda wa maongezi nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages