Mmoja wa waendesha Bodaboda akifungua akaunti ya NMB. |
Waendesha Bodaboda katika picha ya pamoja baada ya semina iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za Wilaya ya Kisarawe. |
Kampeni ya MastaBoda inayoendeshwa na Benki ya NMB kwa ajili ya kuwaunganisha waendesha Bodaboda katika mfumo wa kibenki wa kupokea malipo kwa Mastercard QR kutoka kwa wateja wa Benki ya NMB, Benki zilizounganishwa na Mastacard QR pamoja na mitandao ya simu iliyounganishwa na huduma ya Mastercard QR sasa imevuka boda hadi Kisarawe Mkoani Pwani.
Akizindua kampeni hiyo na kufunga mafunzo ya siku sita yaliyotolewa na NMB kwa waendesha Bodaboda Wilayani humo, Mkuu wa Wilaya Jokate Mwegelo amesema kampeni hiyo imefika muda muafaka katika Wilaya yake.
Jokate amesema, kama Wilaya na Serikali wamejipanga kuipokea kampeni hiyo kwa waendesha bodaboda 150 waliyozitokeza katika mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment