Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Biashara ya DCB, pampja
na wakimbiaji wengine wakipasha viungo wakati wa mashindano ya Familia Marathon
yaliyofanyika katika viwanja vya Chumvi, Bahari Beach jijini Dar es Salaam hivi
karibuni. DCB ilidhamini tukio hilo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Biashara ya DCB walioshiriki
mbio za Familia Marathon wakionyesha medali zao mara baada ya mbio hizo katika
viwanja vya Chumvi, Bahari Beach jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Tukio hilo
lilidhaminiwa na DCB.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Biashara ya DCB walioshiriki
mbio za Familia Marathon pamoja na wakimbiaji wengine wakishangilia mara baada
ya kumalizika kwa tukio hilo katika viwanja vya Chumvi, Bahari Beach, Dar es
Salaam hivi karibuni. Tukio hilo lilidhaminiwa na DCB.
Na mwandishi wetu,
BENKI ya Biashara ya DCB
imezihamasisha familia kujenga tabia ya kushikiri mazoezi ya viungo ili kuweza
kuwa na taifa lenye watu wenye afya bora jambo muhimu katika shughuli za
uzalishaji mali za kila siku.
Akizungumza na washiriki wa mbio
zilizopewa jina la Familia Marathon katika viwanja vya chumvi, Bahari Beach,
nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam hivi karibuni, Mkuu wa Mawasiliano na
Masoko wa DCB, Rahma Ngassa alisema ni muhimu kufanya mazoezi ili kuupa
mwili afya na nguvu na kuzalisha mali.
“Ni ukweli usiopingika kuwa
magonjwa mengi yasiyo ya kuambukiza huchangiwa kwa kiasi kikubwa na aina
ya maisha tunayoishi na uzito mkubwa, mazoezi ya mwili yanasaidia sana
kupambana na hali hizo”, alisema.
Bi Rahma aliongeza kuwa ili tuweze
kuendelea na pia kutimiza azma ya serikali yetu ya kuwa na uchumi wa kati
unaotegemea viwanda, tunahitaji sana kuwa na rasilimali watu wenye nguvu na
afya bora ya kuweza kuzalisha mali kwa wingi.
Mkuu huyo wa mawasiliano alisema
ndio maana DCB ilipopata maombi ya kudhamini Familia Marathon walipokea maombi
hayo kwa mikono miwili kwani kutokana na umuhimu wa mazoezi kwa afya za wateja
wao na watanzania kwa ujumla.
“Wateja wetu wakiwa na afya bora
wataongeza kasi ya uzalishaji mali hivyo hata nasi benki tutanufaika kutokana
na kuwa kwa wateja wetu wafanyakazi, wakulima na wafanyabiashara kwani biashara
zao zikikua na benki inakuwa.
“Endapo tukiwa na watanzania wenye
afya bora, tutapunguza mzigo wa ghara za matibabu kutoka ngazi ya familia hadi
kwa serikali, natoa wito kwa watanzania kujitokeza kwa wingi na kuwa na
utamaduni wa kushiriki mazoezi ya mwili ili kujenga afya bora ya miili yao”,
aliongeza Bi Rahma.
Sambamba za hayo Bi Rahma
alisema licha ya kujali afya ya wateja wao na watanzania kwa ujumla, DCB
imeendelea kutoa fursa na bidhaa mbalimbali kwa wateja zinazolenga kutoa
suluhisho la mahitaji ya kifedha kwa wateja wao. “Bidhaa hizi zinawalenga
wateja wetu wote wakubwa kwa wadogo, wafanyabishara wakubwa na wadogo, wakulima
pamoja na wateja katia makundi mengine”,alisema.
Alizitaja bidhaa hizo kama DCB
Sokoni inayolenga kumkomboa mkulima na mfanyabiashara wa kilimo katika
mnyororo wake wa thamani, DCB Skonga, ikilenga kuwasaidia wazazi katika
suala zima la ada za watoto wao, DCB Lamba Kwanza ambayo mteja huanza hupata
riba nzuri mara anapoamua kuwekeza, DCB kibubu ambayo mteja hujiwekea akiba
mwenyewe kidogo kidogo huku ikianzisha huduma ya DCB Digital ambayo pamoja na
mambo mengine humuwezesha mteja kufungua kaunti mahali alipo na kweza kupata
huduma nyingi za kibenki za DCB kwa njia ya kidigitali.
No comments:
Post a Comment