A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, December 20, 2019

BENKI YA DCB YAZINDUA MKOPO WA ADA YA SHULE

Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Biashara ya DCB, James Ngaluko (wa pili kulia), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya mkopo maalumu wa ada ya shule jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa DCB Skonga, Zamaradi Mketema, Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa DCB, Rahma Ngassa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Fortunata Benedict.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Biashara ya DCB, Fortunata Benedict (kulia), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya mkopo maalumu wa ada ya shule jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa DCB, Rahma Ngassa na Mkurugenzi wa Biashara wa benki hiyo, James Ngaluko.
Balozi wa bidhaa ya DCB Skonga ya Benki ya Biashara ya DCB, Zamaradi Mketema (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya mkopo maalumu wa ada ya shule jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni, Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa DCB, Rahma Ngassa, Mkurugenzi wa Biashara wa benki hiyo, James Ngaluko na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Fortunata Benedict.
Dar es Salaam 19 Disemba, 2019 - Benki ya Biashara ya DCB imezindua huduma ya mkopo maalumu wa Ada ya Shule ikiwa ni fursa nyingine tena itakayowawezesha wateja wa benki hiyo kulipa ada za watoto wao kwa wakati na uhakika.

Mkopo wa ada wa DCB ni mwendelezo wa mkakati wa benki kubuni huduma na bidhaa bora zinazowanufaisha wateja. Benki imekuja na bidhaa hii ya mkopo wa ada katika harakati ya kuwaondolea hofu wazazi linapokuja suala zima la elimu kwa watoto wao hii ni sambamba na akaunti ya DCB Skonga inayomuwezesha mtoto kusomeshwa pindi mzazi anapopata ulemavu wa kudumu ama kifo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi rasmi wa mkopo huu, Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano Bi Rahma Ngassa alisema "DCB inaendelea kuleta kwenye soko bidhaa zinazo kidhi maisha ya watanzania, benki hii ni ya watanzania hivo ni lazima kuja na fursa inayowawezesha wateja wetu kunufaika na benki yao.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages