Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, na wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (MB)akihutubia wageni waalikwa wakati wa hafla yaTuzo ya mwaajiri bora wa mwaka 2019 iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam jana hafla hiyo iliyoudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Naibu Waziri wa Stella Ikupa (MP) pamoja na Taasisi mbalimbali.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, na wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (MB)akitoa juzo kwa mwajiri bora wa mwaka 2019 Mwakilishi kutoka kampuni ya TBL David Magese wakati wa hafla yaTuzo ya mwaajiri bora wa mwaka 2019 iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam jana hafla hiyo iliyoudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Naibu Waziri wa Stella Ikupa (MP) pamoja na Taasisi mbalimbali. Wanaoshuhudia kushoto ni Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt. Aggrey Mlimuka na Mwenyekiti wa Bodi wa chama hicho Jayne Nyimbo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, na wenye Ulemavu Mh. Stella Ikupa (katikati), akitoa tuzo kwa mwajiri bora wa mwaka 2019 kwa nafasi ya mshindi wa pili Mwakilishi kutoka Geita Gold Mine Elizabeth Karua, wakati wa hafla yaTuzo ya mwaajiri bora wa mwaka 2019 iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam jana hafla hiyo iliyoudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Naibu Waziri wa Stella Ikupa (MP) pamoja na Taasisi mbalimbali. anaeshuhudia (kulia), ni Mwenyekiti wa Bodi wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), Jayne Nyimbo katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, na wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (MB).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, na wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (MB)akitoa Cheti kwa Kaimu Mkurugenzi Rasilimaliwatu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Edna Chogo (kulia), wakati wa hafla yaTuzo ya mwaajiri bora wa mwaka 2019 iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam jana hafla hiyo iliyoudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Naibu Waziri wa Stella Ikupa (MP) pamoja na Taasisi mbalimbali. Wanaoshuhudia kushoto ni Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt. Aggrey Mlimuka na Mwenyekiti wa Bodi wa chama hicho Jayne Nyimbo.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na wenye ulemavu, Jenista Mhagama amewataka waajiri nchini,
kuhakikisha wanawawezeshewa fanyakazi waokwenda kuhudhuria mafunzo mbalimbali ili
waweze kupata ujuzi unaohitajika nautakaokidhi ushindani katika mazingira ya kibiashara.
Mhagama ameyasema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati wa hafla
ya utoaji tuzo za waajiri bora wa mwaka kwa mwaka 2019, tuzo zilizoandaliwa na
Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).
Waziri alisema wafanyakazi wakipata mafunzo hayo watajiongeza
ujuzi, watafanyakazi kwa bidii na kuongeza uzalishaji mahali pakazi kwa lengo
la kupambana na manadiliko ya teknolojia.
"Sisisote ni mashahidi mabadiliko ya teknolojia ni makubwa
kwelikweli, kwahiyo kama hatutawashirikisha wafanyakazi wetu kupata ujuzi mpya na
mafunzo endelevu katika maeneo yetu ya kazi ambayo yatawasaidia kuendana na mabadiliko hayo yateknolojia katika ulimwengu,
tunaweza tukajikuta hatupigi hatua kwenda mbele na hatutaweza kufikia malengo tuliyojiwekea
ndani ya taasisi zetu na taifa kwa ujumla," alisema.
Alisema pia anawakumbusha waajiri kuendelea kuchangia katika mfuko
wa fidia kwa wafanyakazi kwani umekuwa ukiwakinga waajili na madhala na majanga
wanayoyapata mahali pa kazi.'
Uchangiaji katika mfuko huu unamanufaa makubwa situkwawafanyakazi
hata kwa waajiri kwani utamsaidia mwajiri kuwa na nguvukazi yenyeafya njema itakayofanyakazi
kwa kujiamini," alisema
Aidha alisema wanapoendelea kuijenga nchihasa katika kuwekeza
kwenye sekta ya viwanda wanategemea kwa kiasi kikubwa mchango wa sekta binafsi kama
injini ya kujenga uchumi hivyo maamuzi ya ATE ya kutambua na kuwekeza katika rasilimali
watu nikuongeza tija kwenye maeneo ya kazi.
Aidha alisema wao kama serikali, waajiri na Chama cha
wafanyakazi nchini (Tucta) watahakikisha kwamba tuzo hizo zinaendelea kilamwaka
bilakukoma kwani nichachu kwa waajiri katika kuleta mabadiriko mahala pa kazi.
Naye Naibu Waziri Ofisiya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Stella Ikupa amewataka waajiri kuendelea kuunga
mkono juhudi za serikali katika kuwasaidia watu wenye ulemavu vifaa visaidizi
"Vifaa visaidizi kwa watu wenye ulemavu nikama chakula maana
vinahitajika kila siku.
Unapomnunulia mtu mwenye ualbino mafuta yataisha na atahitaji
mengine baada ya muda hivyo ni muhimu sana kwa wadau kujitokeza kwawingi kununua
vifaa hivyo vikiwamo fimbo kwa wasiona na Wheel Chair
(vitivyawalemavu),"alisema
Kwa upande wake Ofisa Mtendajiwa ATE, Agrey Mlimuka alisema tuzo
hizo zilianza kutolewa mwaka 2005 zimekuwa zikihamasisha kampuni wanachama kuweka
juhudi katika masuala ya ajira na usimamizi warasilimaliwatu kama msingi na mkakati
wa kujenga nguvu kazi yenye ujuzi, furaha na ushindani.
Alisema kutokana na mapendekezo yaliyotolewa, kwa mwaka huu tuzo hiyo ya mwajiri bora imeongeza vipengele vipya vitatu hivyo kufanya
kuwa na jumla ya vipengele 38 kutoka 35 vilivyokuwepo mwakajana.
Vipengele vilivyoongezeka ni mwajiri bora anayeendeleza mafunzo
ya ujuzi kwa Kazi kwa wahitimu, mwajiri bora anayetoa mafunzo ya uwanangezi pamoja
na tuzo ya mwajiri bora anayezingatia haki rasilimali, haya yaliku wamaagizo ya
waziri mwakajana na tumeyatekeleza.
Alisema lengo la kuongeza vipengele hivyo nikuendelea kuboresha
tuzo hizo, kuongeza ushindani miongoni mwawashiriki pamoja na kugusa kila eneo ambalo
litaleta tija katika ukuzaji na uendelezaji warasilimaliwatu katika maeneo ya kazi.
"Tunatambua bila rasilimali watu hatuwezi kupiga hatua wala
kwenda kwenye uchumi wa viwanda tunao usema, hivyo tuzo hizo mpya ni nyongeza katika
zile zinazotolewa ambazo ni utawala na uongozi, ubora na usimamizi warasilimaliwatu,
bidhaa na huduma, uwajibikaji katika mwenendo wa biashara, pamoja na usalama wa
mwajiri wakati eneo la kazi”
Alisema wameendelea kuwa na tuzo ya mshindi wa jumla na kuongeza
kuwa ushiriki wa kampuni katika tuzo hizo umeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka
kutokana na ukweli kwamba ni jambo muhimu kwa ustawi wa wafanyakazi.
Kwa upande wake Mwenyekitiwabodiya ATE, Jayne Nyimbo alisema wanaomba
wapate fursa ya kukutana na Rais John Magufuli kwani tangu aingie madarakani hajapata
nafasi ya kukutana na waajiri ili kujua changamoto wanazo kumbananazo.
Alisema ATE wanaamini kuwa
iliwafikie mafanikio hasa katika Nyanja za kiuchumi na kijamii ni muhimu kuzingatia
mgawanyo sawa warasilimali zao nchini kwa watu wote.
"Kwa kuzingatia hilo waajiri tunaendelea kutekeleza
program maalum ya Female ambayo inalengo kuwajengea uwezo wanawake na hicho kuwawezesha
kushika nafasi za uongozi katika Nyanja mbalimbali katika taifa letu, natoa wito
kwa waajiri waendelee kushiri kikatika mpango huu ili kujenga mazingira yanayo
jail usawa wa kijinsia hasa katika ngazi za maamuzi," alisema.
No comments:
Post a Comment