A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, December 10, 2019

Amber Rutty Atangaza Kuwa Singo, “Jimbo Liko Wazi”

DAR: Msanii na video vixen matata asiyeishiwa vituko Bongo, Rutyfiya Abubakar ‘Amber Rutty’, ametangaza kuwa yupo ‘singo’ na kuibua gumzo kama lote. Kufuatia kutangaza ishu hiyo, ina maana kuwa ameachana na aliyekuwa mpenzi wake aitwaye Said Mtopali.
Amber Rutty ametangaza kuwa jimbo lipo wazi kupitia ‘status’ za Mitandao ya Kijamii ya WhatsApp na Instagram ambapo ameandika;

“Hongera zao walioolewa jamani duh, kama ndoa zenyewe ndiyo hivi, nimeshindwa, kumbe wanaodanga wanajua wanachokifanya kina maana gani loh, hebu nipumue zangu na mimi nipate danga jipya mjini, Mungu atanionesha njia sahihi Inshalaah!”
Wawili hao walikuwa kwenye ndoa kwa mwaka mmoja na walianza uhusiano wao miaka sita iliyopita.
Hata hivyo, kinachoibua mshtuko ni kutokana na jinsi ambavyo Amber Rutty amekuwa akitangaza kumpenda jamaa huyo na kwamba hawezi kuachana naye huku wakiendelea kumtafuta mtu ambaye aliyevujisha video zao zilizokosa maadili, ambazo ziliwafanya kuwekwa ndani na kupandishwa mahakamani.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages