A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, October 3, 2019

Yanga kumkosa leo kocha wao Zahera


Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo inaendelea, Yanga itakuwa nyumbani (uwanja wa Uhuru) kucheza na Polisi Tanzania ya Kilimanjaro.

Yanga imecheza mchezo mmoja tu wa ligi na kupoteza kwa kufungwa goli 1-0 na Ruvu Shooting palepale kwenye uwanja wa Uhuru.

Polisi Tanzania ilishinda mchezo wake wa kwanza wa ligi dhidi ya Coastal Union lakini ikapoteza mchezo uliopita kwa kufungwa na Ruvu Shooting.

Yanga leo itamkosa kocha wake mkuu Papaa Zahera Mwinyi ambaye ataanza kutumikia adhabu ya kufungiwa kukaa kwenye benchi kwa mechi tatu kufuatia kuvaa mavazi ambayo si nadhifu kinyume na kanuni za ligi.

Baada ya kuikosa michezo miwili ya CAF Champions League kwa sababu za kikanuni, Yanga jana ilithibisha leo Molinga ataongoza safu ya ushambuliaji kwenye mchezo dhidi ya Polisi Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages