Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa kampuni ya Selcom Baguma Ambarei (kushoto), akizungumza
na waandishi wa habari akitoa mfano wa
kulipia mafuta kwa kutunia Mastercard kwa wamiliki magari wanaotumia vituo vya mafuta ya Puma kwa
ushirikiano Makampuni hayo ambapo mteja atarudishiwa asilimia 5 ya fedha
kwa kutumia kadi hiyo, kutoka (kulia) ni mfanya kazi wa Puma,
Khamis Ali, Mkurugenzi wa Puma, Dominic Dhanah, na Mkurugenzi Mtendaji wa
Selcom Sameer Hirj.
Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom Sameer Hirj
(kushoto), akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya kulipia mafuta kwa
kutunia Mastercard kwa wamiliki magari wanaotumia vituo vya mafuta ya Puma kwa
ushirikiano Makampuni hayo ambapo mteja atarudishiwa asilimia 5 ya fedha
kwa kutumia kadi hiyo (kulia), ni Mkurugenzi Mtendaji wa Puma, Dominic Dhanah.
Mkurugenzi Mtendaji wa Puma, Dominic Dhanah (kulia),
akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya kulipia mafuta kwa kutunia Mastercard
kwa wamiliki magari wanaotumia vituo vya mafuta ya Puma kwa
ushirikiano Makampuni hayo ambapo mteja atarudishiwa asilimia 5 ya fedha
kwa kutumia kadi hiyo kulia kwa Dominic ni Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom Sameer Hirj.
PUMA ENERGY, SELCOM NA MASTERCARD WAUNGANA
KUHAMASISHA MALIPO YA KIELEKTRONIKI.
Dar es salaam, Tanzania; Puma Energy, Selcom Paytech LTD na Mastercard kwa wamezindua kampeni ya pamoja iitwayo #BombaWeekend ambayo inaangalia kurejeshea wateja hadi 5% ya pesa watakayotumia watakapojaza mafuta katika vituo vya Puma Energy endapo watalipia kupitia Mastercard QR.
Dar es salaam, Tanzania; Puma Energy, Selcom Paytech LTD na Mastercard kwa wamezindua kampeni ya pamoja iitwayo #BombaWeekend ambayo inaangalia kurejeshea wateja hadi 5% ya pesa watakayotumia watakapojaza mafuta katika vituo vya Puma Energy endapo watalipia kupitia Mastercard QR.
Kampeni hiyo itaendeshwa kwa wiki 11, kila Ijumaa hadi Jumapili kuanzia
saa 10 hadi 12 jioni kupitia mtandao wa Puma wenye vituo 52 nchi nzima. Pamoja
na dhumuni la kuzawadia watumiaji wa huduma hiyo, Bomba Weekends ina dhamira ya
kuchangia katika juhudi za serikali za kurasimisha malipo na kuhamasisha uchumi
wa malipo ya kieletroniki ili kufikia malengo ujumuishaji wa kifedha wa nchini
Tanzania.
Mchakato mzima wa kurudishia pesa wakati wa Bomba Weekends unaendeshwa
kupitia huduma ya zawadi kwa wateja ya Qwikrewards iliyoundwa na Selcom Paytech
LTD mahususi kwa watumiaji wa Mastercard QR. Qwikrewards inamuwezesha mtu
yeyote kukusanya pointi au kupata pesa taslim kupitia akaunti iliyounganishwa
na namba yake ya simu kila afanyapo malipo kutumia Mastercard QR. Watumiaji
Qwikrewards wanaweza kukomboa pointi walizokusanya kwa kupiga *150*15* na
kuzitumia katika maeneo zaidi ya 30,000 nchini ambapo Mastercard QR inakubalika
kama njia ya malipo. Aidha Mastercard QR imepiga hatua kubwa tangu kuanzishwa
kwake nchini mwaka 2018 hadi sasa kupelekea kukubalika na watoa huduma mbali
mbali zaidi ya 30,000 kuwa na uwezo wa kupokea malipo kutoka mitandao yote 7 ya
simu na benki 15 nchini.
Akiongea na wanahabari katika hafla ya uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji wa
Puma Energy Tanzania, Nd. Dominic Dhanah alisema, "Bomba Weekends
inahamasisha wateja we kulipia mafuta
katika vituo yetu kutumia njia rahisi, haraka na salama zaidi na kunufaika papo
hapo kupitia Qwikrewards kutoka Puma. Ushirikiano huu unadhahiri kwamba Puma ni
kiongozi wa katika sekta ya mafuta inapofikia kujiunga na suluhisho bunifu za
malipo ambazo hurahisisha malipo kwa wateja wetu na kutuwezesha kutoa huduma
bora zaidi katika vitu vyetu."
Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom Paytech LTD, Nd. Sameer Hirji, alionyesha
matumaini makubwa kuelekea uchumi wa malipo ya kielektroniki akisisitiza kuwa
ni lazima taasisi ambazo zinaongoza mchakato huo kuongeza thamani kwa wateja
ili kuwapa hamasa zaidi kutumia malipo ya elektroniki."Kupitia Bomba
Weekends tukishirikaina Puma Energy pamoja na Mastercard QR tumedhamiria
kuwazawadia wateja watakaolipa kielektroniki katika matumizi yao ya kila siku,
mafuta yakiwa sehemu kubwa ya matumizi hayo. Tunaamini kwamba tunavyozidi
kurahisisha na kuimarisha upatikanaji na upokeaji wa malipo ya kieletroniki
ndivyo tutazidi kuwajengea Watanzania imani ya kutoka nyumbani bila pesa
taslim. Tukiwa na Qwikreward na maeneo zaidi ya 30,000 ambapo Mastercard QR
inakubali kitaifa tunaamini tunaongoza mabadiliko kuelekea malipo ya
kielektroniki na malengo ujumuishaji wa kifedha nchini Tanzania.”
Kwa upande wake, Mkuu wa Biashara wa Mastercard Ukanda wa Afrika
Mashariki, Nd. Adam Jones alisema,”Mastercard itaendelea kutoa huduma
shirikishi za malipo ambazo zitasaidia kusukuma jamii kuelekea malipo ya
kieletroniki. Njia sahihi ya kufikia malengo haya ni kuendelea kuvumbua mifumo
thabiti ya kidijitali kwa kushirikiana na mashirika kama Selcom na Puma Energy. Tuna uhakika kampeni hii
itawahakikishia wateja malipo rahisi, salama na ya uhakika katika kila kituo
cha Puma, lakini pia kuchangia juhudi ya nchi kuelekea malipo ya kidijitali.”
No comments:
Post a Comment