A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, October 2, 2019

RC MAKONDA AMUONYA MKANDARASI WA MRADI WA UJENZI NA MABORESHO YA MTO NG'OMBE, ACHUKIZWA NA VIONGOZI WALIOMDANGANYA KAZI INAENDELEA WAKATI HAKUNA CHOCHOTE

WhatsApp%2BImage%2B2019-10-01%2Bat%2B6.07.50%2BPM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo October 01 amefanya ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo Wilaya ya Kinondoni ambapo akiwa katika Mradi wa Maboresho ya Mto Ng'ombe unaogharimu Shilingi Bilioni 32 ukiwa na urefu wa Km 7.5 amechukizwa kuona hakuna chochote kinachoendelea kwenye mradi licha ya Viongozi wa Wilaya kumdanganya kuwa Mkandarasi yupo Site anaendelea na kazi wakati wa kikao kazi kilichofanyika siku 6 zilizopita kwenye ukumbi wa Karimjee.

Kutokana na hilo RC Makonda amemuagiza Mshauri wa Mradi kumuita Mkandarasi huyo Mara moja ofisini kwake ili aeleze nikwanini kazi haifanyiki wakati tayari mkataba umesainiwa tokea 16/06/2019.

WhatsApp%2BImage%2B2019-10-01%2Bat%2B6.07.49%2BPM

Aidha RC Makonda amemuagiza mkandarasi huyo kuhakikisha kazi hiyo inakamilika na kukabidhiwa ndani ya miezi 10 kuanzia sasa tofauti na miezi 18 waliyoomba huku akiwaonya Watendaji wanaoendelea kumpa taarifa za wongo kuwa Yeye, Katibu tawala wa Mkoa huo na Kamanda Mambosasa wataendelea kufanya ziara kwenye kila mradi kujionea kama taarifa wanazoletewa kwenye karatasi zinaendana na kinachofanyika Site.

WhatsApp%2BImage%2B2019-10-01%2Bat%2B6.07.48%2BPM%2B%25281%2529

Akiwa kwenye Mradi wa ujenzi wa Soko la Kisasa Magomeni linalogharimu kiasi cha Shilingi bilioni 8.9, RC Makonda amemtaka mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha Soko hilo linakabidhiwa Mwezi Disemba mwaka huu.

Pamoja na Hayo RC Makonda ameielekeza Manispaa ya Kinondoni kuhitisha kikao na Wafanyabiashara wa soko hilo ili wakubaliane namna ya kuweka jografia ya soko hilo ikiwa ni pamoja na sehemu za maduka,vizimba na eneo la kushusha mizigo.

WhatsApp%2BImage%2B2019-10-01%2Bat%2B6.07.42%2BPM

WhatsApp%2BImage%2B2019-10-01%2Bat%2B6.07.50%2BPM%2B%25281%2529

Pamoja na hayo RC Makonda ametembelea mradi wa Ujenzi wa Soko la Tandale unaogharimu kiasi Cha shilingi Bilioni 8 na kuelekeza Manispaa ya Kinondoni kuhakikisha mkandarasi anafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha anakabidhi kazi ndani ya Miezi sita kuanzia sasa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages