Kumekuwa
na ripoti juu ya baadhi ya wazazi kuwatelekeza watoto wao na kuwafanya wakose
haki zao za msingi kinyume cha sheria.
Wakati
kifungu cha 7 cha Sheria ya Mtoto (2009) kinatoa haki ya mtoto kukua akiwa na
wazazi wake, kifungu cha 8 kinatoa wajibu kwa mzazi, mlezi au mtu yeyote
anayemtunza mtoto na hasa wajibu huu unampa mtoto haki ya kupata chakula,
malazi, mavazi, huduma ya afya, ikiwa ni pamoja na kupata chanjo, elimu na
mwongozo, uhuru na haki ya kucheza na kupumzika. Hata hivyo, yote haya
hayafanyiki kwa baadhi ya familia nchini.
Mtoto
wa kike mwenye umri wa miaka miwili, Victoria Dotto, aliyezaliwa Wilaya ya
Malinyi alitelekezwa hivi karibuni na mama yake Joyce Ishengela na haijulikani
mahali mama huyo alipo na hakuna anayejua sababu zilizomfanya amtelekeze mtoto
wake.
Bi Ishengela, ambaye pia ametelekezwa na mume wake kwa muda sasa,
alizaliwa Mkoa wa Mwanza mwaka 2002. Alienda kwa dada yake Bi Mbuke Madini
Wilaya ya Malinyi akiwa na mtoto wake, ambaye alimtelekeza baadaye.
Mpita
njia mmoja, Bw Ally Mkutila, alimkuta mtoto huyo akiwa peke yake alipokuwa
akienda kulima shambani kwake. Njia aliyopita ilikuwa karibu na nyumba ya Bi
Madini, ambapo mtoto huyo aliachwa bila ya kuwa na mwangalizi yeyote.
Bw
Mkutila alishangaa kwa nini mama amwache mtoto wake katika mazingira kama yale
na hivyo alimjulisha msaidizi wa kisheria baada ya kuona mtoto yuko kwenye
mazingira yasiyo rafiki na salama kwa mtoto.
Baada
ya Bw Mkutila kutoa habaria Kituo cha Wasaidizi wa Kisheria Malinyi, mmoja wa
wasaidizi wa kisheria alienda kumwona mtoto huyo na kumkuta katika mazingira ya
hatari.
“Nilimkuta
mtoto kwenye mazingira hatarishi. Hapakuwa na mtu wa kumsaidia mtoto nilipofika
nyumbani hapo. Niliuliza mahali alipo mama yake na hakuna mtu aliyejua
alipoenda,” alisema msaidizi wa kisheria Bi Martha Elimba, aliyeamua kumchukua
mtoto huyo hadi kituoni kwao. “Mtoto alikuwa bado mchanga kuachwa katika mazingira
yale peke yake.” Bi Elimba alitoa taarifa Ofisi ya Ustawi wa Jamii wilayani kwa
hatua zaidi.
Kituo
cha Wasaidizi wa Kisheria Malinyi, kwa ushirikiano na Ofisi ya Ustawi wa Jamii
Wilaya ya Malinyi, kilimjulisha Mkurugenzi wa Wilaya ya Malinyi Bw Musa Mnyeti
juu ya mtoto aliyetelekezwa na mkurugenzi akatoa kiasi cha shilingi 180,000 kwa
ajili ya kusaidia matunzo ya mtoto. Baadaye mtoto huyo alipelekwa Hospitali ya
Lugala ya Kanisa la Kilutheri Wilaya ya Malinyi.
Ofisi ya Ustawi wa Jamii iliandika barua ya utambulisho kwa wasaidizi wa
kisheria ili kurahisisha mapokezi ya mtoto.
Daktari
wa hospitali hiyo Emmanuel Chogo alimpokea mtoto na baada ya uchunguzi
alishauri mtoto alazwe na kubaki hospitalini hapo hadi atakapofikisha uzito wa
kilo 9 kwani alionekana kuwa na uzito chini ya wastani kwa sababu ya ukosefu wa
lishe bora.
Habari
zinasema, motto huyo sasa hivi anaendelea vizuri, asante kwa msaada na
ushirikiano ulifanywa na msamaria wema, wasaidizi wa kisheria, mkurugenzi wa
wilaya, daktari wa hospital ya Lugala, Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, na wote
walihusika kumsaidia motto huyo.
No comments:
Post a Comment