Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizungumza jambo wakati alipokutana na walimu na wanafunzi wao wakati akiwatunuku vyeti na zawadi mbalimbali.
… Paul Makonda akionesha msisitizo wa jambo mbele ya wakuu wa shule za msingi na sekondari pamoja na walimu.
… Makonda akiwatunuku vyeti wakuu wa shule zilizofanya vizuri katika mitihani yao ya Taifa.
…Wakiendelea kupokea vyeti vya ushindi.
Mmoja wa wakuu wa shule akionyesha cheti alichokipokea kutokana na ushindi wa shule yao.
Amesema katika mkutano huo utakaofanyika Jumatano ya September 25 Ukumbi wa Karimjee mtendaji atakaebainika kusababisha uzembe huo atawajibisha hapohapo kwa mujibu wa sheria na wengine watazuiwa mishahara yao.
Aidha ametoa wito kwa Wizara ya Utumishi na TAMISEMI kutafuta njia bora ya kuwapata wakuu wa Idara wenye uwezo wa kuleta matokeo Chanya tofauti na sasa ambapo wengi wao wamepanda na kuwa wakuu wa idara kwa kigezo cha kukaa kazini Muda mrefu.
Hayo yote yamejiri leo wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa walimu, wanafunzi na shule zilizofanya vizuri katika taaluma na Michezo.
No comments:
Post a Comment