Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo September 23 ametembelea na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Stand mpya ya kisasa ya Mabasi ya Mikoani na Nchi za Jirani ya Mbezi Luis ambayo ujenzi wake umefikia 35% hadi sasa na Kumtaka Mkandarasi kukamilisha Ujenzi huo kwa wakati.
Amesema ujenzi wa Stand hiyo utagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 50.9 ambapo ndani yake kutakuwa na huduma zote muhimu ikiwemo Jengo la Abiria,Utawala, Maegesho ya mabasi 500, Shopping Mall, Hotel, Maegesho ya Taxi, Bajaji, Pikipiki, Bank, Petrol station, Apartment, ofisi za mabasi, sehemu ya wafanyabiashara, mama Lishe,Vyoo, Kituo cha Polisi na sehemu ya kuhifadhi mizigo.
Aidha amemuelekeza katibu Tawala wa Mkoa huo kuunda Kamati ya kufuatilia Maslahi ya wafanyakazi wote wanaofanya kazi katika miradi ya kimkakati ili kuhakikisha wanapata stahiki zao zote ikiwemo mishahara na mifuko ya hifadhi ya jamii.
Pamoja na hayo ameendelea kuwataka wakandarasi wa miradi mbalimbali kuhakikisha wananunua vifaa kutoka kwenye Viwanda vya wazawa jambo litakalosaidia kuinua uchumi wa Viwanda na Taifa kwa ujumla.
Katika Ziara hiyo ameambatana na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment