Kampeni ya Matibabu ya Upasuaji wa Moyo kwa Watoto 10 kila mwezi kwa muda wa miezi Sita kutoka familia duni iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda imeendeleakuwa na mafanikio makubwa ambapo Balozi wa Jumuiya ya Falme za Kiarabu UAE Bw.Khalfan Abdulrahman Al-Mazouqi amemuunga mkono kwa kuleta madaktari bingwa wa kufanya upasuaji kwa watoto hao.
Amesema Balozi huyo ameamua kujitolea Madaktari hao baada ya kuona kipande cha Video kikimuonyesha RC Makonda akiwa yupo kwenye wodi ya watoto wenye matatizo ya moyo kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya jambo lililomgusa balozi na kuamua kumuunga mkono kwenye kampeni hiyo.
Aidha amesema kuwa hadi sasa jumla ya watoto 30 kati ya 60 wamefanyiwa upasuaji kwa kipindi cha miezi mitatu huku akitoa wito kwa wananchi na wadau kugusa maisha ya wenye uhitaji kwa kuwafika taasisi ya moyo Jakaya Kikwete na Kujitolea kugharamia upasuaji kwa watoto kwahuwa hadi sasa kuna zaidi ya watoto 500 wenye tatizo la moyo lakini wazazi hawana uwezo wa kumudu ghrama za matibabu.
No comments:
Post a Comment