A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Sunday, August 4, 2019

RC MAKONDA AWAPA ULAJI WACHONGA VINYAGO NA WACHORAJI PICHA, AWAKABIDHI SEHEMU YA KUUZA BIDHAA KWA WAGENI ZAIDI YA 1,000 KUTOKA SADC

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akizungumza na wafanya biashara pamoja na wasanii wa uchongaji naUchoraji wa Mwenge Vinyago wakati alipokwenda kuwatembelea na kufanya nao mazungumzo.
Baadhi ya wafanya biashara wa Mwenge vinyago wakiwa katika mkutano huo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ametangaza kuwa ifikapo August 06 atafunga Barabara zinazozunguka Chuo cha IFM zenye ukubwa wa Mita 700 ili eneo hilo litumiwe na Wachonga vinyago, Wachoraji wa picha na watengeneza Shanga kuuza bidhaa wanazozalisha kwandani ya siku 15 za ugeni wa viongozi wa Jumuiya ya SADC.

Amesema kwakuwa eneo hilo lipo jirani na Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere unapofanyika mkutano huo itakuwa rahisi kwa wageni kutembelea wafanyabiashara hao na kununua bidhaa mbalimbali zinazatengenezwa kwa umahiri na ubunifum mkubwaikiwemo Vinyago, Picha za kuchora, Shanga na Vinyago jambo litakalosaidia pia kutangaza utalii wa Tanzania.

Aidha amesema eneo hilo pia litakuwa na ulinzi wa kutosha na litafungwa Taa za kisasa ili kuhakikisha wageni wafika na kununua bidhaa muda wowote kwa kipindi chote cha mkutano wa Jumuiya ya SADC jambo litakalosaidia kukuza uchumi wa wauzaji na Taifa kwaujumla.

Hata hivyo amesema ni vyema Wananchi wakauchukulia Ugeni huu wa Viongozi zaidi ya 16 wa Jumuiya ya SADC kama sehemu ya fursa ya kuuza na kutangaza bidhaa zao.

Mkuu wa Mkoa akikagua baadhi ya picha zilizocjorwa na wasanii hao


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages