A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, August 17, 2019

Mjadala wa kuongeza muda wa uongozi kwa Rais Magufuli, Polepole afafanua


Mjadala wa kuongezewa muda wa uongozi Rais Magufuli, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, amewataka wanachama wa chama hicho kutoendelea na mjadala huo kwa kuwa unamkwaza kiongozi huyo.

Polepole alisema aliitwa na Rais Magufuli ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho na kumtaka awatangazie Watanzania kwamba nchi inaongozwa kwa Katiba na sheria hivyo amesikia watu wakizungumza kuhusu kuongezewa muda baada ya kumaliza ukomo wa muda wa uongozi wake jambo ambalo linamkwaza.

Alisema hayojijini Dodoma wakati  akifungua kikao cha Baraza la Jumuiya ya Wanawake wa Chama hicho (UWT).

“Wale wanachama wenzangu ambao mnaendeleza huu mjadala wa kuongezwa muda wa uongozi naomba muuache maana mwenyekiti anasema anakwazwa nao,”alisema.

Kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Polepole alisema katika mchakato wa kuteua wagombe, wajiepushe kuteua watu ambao ni walaghai na wasio kubalika na jamii kwa kuwa inawavunja moyo wanawake.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages