A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, August 17, 2019

Ali Kiba, Harmonize walivyopishana kwenye msiba wa Mbalamwezi

Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Ali Kiba na Harmonize wamepishana katika msiba wa msanii, Abdallah Matimbwa maarufu Mbalamwezi wa kundi la The Mafik.

Tukio hilo limetokea leo katika msiba wa msanii huyo ambaye kwa mujibu wa rafiki zake alitoweka katika sikukuu ya Eid na siku nne baadaye polisi walitoa taarifa za kupatikana kwa mwili wake.

Katika msiba uliokuwa Tandika mtaa wa Mindu jijini Dar es Salaam, Ali kiba alifika saa sita mchana na saa moja baadaye Harmonize naye alifika eneo hilo, kuanza kusalimiana na wasanii mbalimbali.

Dakika chache baada ya msanii huyo wa kundi la WCB  kufika, Ali Kiba aliyekuwa ameketi na wasanii wengine akiwemo Fid Q alinyanyuka na kuaga wasanii wa kundi la The Mafik, Hamadai na Rhino King na kuondoka.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages