A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, July 18, 2019

WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI KUTOKA JAMHURI YA CZECH WATAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NCHINI TANZANIA

Mhe. Dkt. Abdallah Saleh Possi, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani ambaye pia ni Balozi wa Tanzania asiye na makazi nchini Czech akiwa kwenye mkutano kati ya ujumbe wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) uliofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 15 Julai 2019. Mhe. Balozi Possi ameambatana na ujumbe huo hapa nchini ambao una lengo la kutafuta fursa za biashara na uwekezaji kwenye sekta za afya, kilimo, nishati na madini na ujenzi wa viwanda vya madawa na vifaa tiba. 
Sehemu ya Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech ukufuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa kwao na Wataalam kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Sehemu nyingine ya Wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech.
Mkutano ukiendelea.
Mhe. Balozi Possi (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa TIC na wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech.
Ujumbe wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech wamewasili nchini tarehe 13 Julai, 2019 kwa lengo la kukutana na kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali nchini ili kujadili fursa za biashara na uwekezaji nchini katika sekta mbalimbali hususan afya, kilimo, miundombinu ya barabara na reli,nishati, madini,utalii na wa ujenzi wa viwanda vya madawa na vifaa tiba.

Ziara hiyo inatokana na juhudi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Ubalozi wa Tanzania uliopo nchini Ujerumani ambao pia unawakilisha Tanzania katika Jamhuri ya Czech na wadau wengine muhimu katika kushawishi wafanyabiashara wakubwa kuja kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages