Balozi wa M-Pawa kupitia Benki ya
CBA Silvery Mujuni, maarufu kama Mpoki
(kushoto),
akiongea kwa njia ya simu na mmoja ya Mshindi wa M-Pawa kupitia Benki hiyo wakati
wakuchezesha droo ya pili ya kukopa na kuweka na M-Pawa inayoendelea katika
kusherehekea miaka 5 ya huduma hiyo nchini. Droo hiyo imefanyika katika ofisi
za makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam leo. Wengine ni Mwakilishi
kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Jehud Ngolo, pamoja Dokii Stanslaus Picha na Brian Peter
CBA/Vodacom wamefanya droo yao
ya pili ya promosheni yao ya Kukopa na kuwekeza na M-Pawa inayoendelea katika
kusherehekea miaka 5 ya huduma hiyo nchini. Droo hiyo imefanyika katika ofisi
za makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam.
Washindi wa droo ya pili
walitangazwa mbele ya mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Bwana.
Jehud Ngolo, afisa mwandamizi wa ukaguzi, wafanyakazi wa benki ya CBA pamoja na
wachekeshaji maarufu Silvery Mujuni ‘Mpoki’ na ‘Dokii’.
Washindi hao walichaguliwa
kutoka makundi 3 ambayo ni kuweka akiba, kulipa mkopo mapema pamoja na Savings
challenge na walipata mara 2 ya akiba iliyopo kwenye akaunti zao ambayo ina
kianzio cha kati ya Tsh 1000 hadi laki 2, washindi wengine wenye pesa zaidi ya
laki 2 wamepata mara 2 ya kiasi hicho. Washindi wengine wa marejesho ya mkopo
na Savings challenge wamezawadiwa simu pamoja na muda wa maongezi.
Huduma ya M-Pawa inalenga zaidi
kuwajali wateja wake na itaendelea kutoa zawadi mbalimbali katika kipindi hiki
cha pomosheni huku tukijidhatiti katika kuboresha huduma zetu za kifedha na
kujumuisha wateja wetu, alisema Bibi. Zainabu Mushi mwakilishi kutoka benki ya
CBA wakati wa kuendesha droo hiyo.
Tunawahimiza watumiaji wote wa huduma ya
M-Pawa washiriki kwenye promosheni hii kwa kuweka akiba, kukopa na kurudisha
mikopo yao mapema ili kujiweka kwenye nafasi ya kushinda pamoja na kuwahimiza
watu wengine wasiotumia M-Pawa kuanza kutumia huduma hii.
No comments:
Post a Comment