A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, June 13, 2019

TFF kutangaza benchi la ufundi kwa Serengeti Boys


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limethibitisha kuachana rasmi na Mkurugenzi wake wa Ufundi Ammy Ninje kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kubanwa na majukumu ya kifamilia baada ya kumaliza muda wake.

Rais wa Shirikisho hilo Wallace Karia amesema Ninje anarejea nchini Uingereza na wakati wowote kuanzia sasa watamtangaza mkurugenzi mpya pamoja na msimamizi mkuu wa benchi la ufundi la timu ya vijana U17 Serengeti Boys.

Kwa upande wake, Ninje amekiri kuwa suala la familia ndilo lililomfanya ajiondoe kwenye soka la Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages