A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, June 20, 2019

RC Makonda awatoa hofu Watanzania kuhusu tishio la ugaidi


Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa hakuna tishio lolote lile, ni vyema watoa taarifa wakazingatia Katiba ya nchi.

Makonda amewatoa hofu wananchi kuwa hali ya jiji la Dar Es Salaam ni shwari na hakuna tishio lolote katika Mkoa huu.

“Nimelazimika kuja kwenu usiku huu, niwatoe hofu walioko kwenye Mahoteli kwamba hakuna tishio lolote lile, ni vyema watoa taarifa wakazingatia Katiba ya Nchi yetu kwani tunavyo Vyombo maalum vya kutangaza kama kuna hali ya hatari,” Paul Makonda.

Kauli ya Makonda inakuja baada ya Ubalozi wa Marekani Tanzania kutahadharisha fununu za uwezekano wa mashambulizi ya kigaidi Masaki Dar kwenye Hoteli/Migahawa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages