A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, May 23, 2019

PICHA: Patoranking afanya Listening Party ya albam yake mpya "Wilmer", mastaa kibao waibuka


Ni jambo la kawaida kwa wasanii wakubwa wanapotaka kuachia albam zao lazima wafanye sherehe ya kuwaalika watu wao wa karibiu kuweza kuisikiliza kwa mara ya kwanza (Listening Party) kabla ya kutua kwa mashabiki.

Patoranking moja ya wasanii wakubwa Afrika Jumanne ya wiki hii amefanya sherehe kama hiyo kwa ajili ya albam yake ya WILMER ambayo inatarajiwa kuachiwa Mei 24 ya mwaka huu ikiwa ni siku tatu kabla ya sherehe yake ya kuzaliwa.

Sherehe hiyo ilifanyika  Lagos, Nigeria, na kuhudhuriwa na mastaa kibao akiwemo Wizkid, Don Jazzy, D'Banj, Tiwa Savage, Seyi Shay, Run Town, Yemi Alade, Phyno na wengine.


Albamu ya WIMER imepewa jina la mtoto wake ambaye amezaliwa hivi karibuni na ina ngoma 12 akiwa amewashirikisha jumla ya wasanii sita akiwemo Davido kwenye wimbo uliopewa jina la "Confirm" ambao ni wamwisho kwenye albamu hiyo.

WILMER ni albam ya tano ya Patoranking tangu alipoanza rasmi muziki mwaka 2009. 
Hapa chini picha zaidi za tukio hilo.








No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages