A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, April 23, 2019

Waziri Mkuu awataka Mawaziri wajiandae kwa hili



Waziri Mkuu amewataka mawaziri walioko Mtumba wajiandae kwani kuna siku atakwenda kufanya vikao vyake kwenye wizara zao kwa sababu amebaini kuwa kila wizara ina ukumbi mkubwa wa mikutano.

Ametoa kauli hiyo (Jumanne, Aprili 23, 2019) wakati akitoa majumuisho ya ziara hiyo fupi kwa maafisa wa Serikali waliokuwepo kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara ya nishati ambako ndiko alimalizia ziara yake.

Mapema, akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alisema jumla ya watumishi 64 wameshamia kwenye ofisi za wizara hiyo ambapo kuna vyumba 25 vya ofisi na ukumbi mmoja wa mikutano.

Pia alisema waligawa miche ya miti 13,570 kwa wizara mbalimbali na kwamba katika ofisi yake, wamepanda miti 980.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi (OR-TAMISEMI), Bw. Suleiman Jafo alisema wamekwishahamia tangu Jumatatu iliyopita na kwa sasa wanatumia ofisi za muda ambazo ni za mabati huku wakisimamia ujenzi wa ghorofa yao hadi ukamilike.


Akielezea kuhusu ujenzi wa ofisi hizo ulipofikia, Bw. Jafo alisema ifikapo mwishoni mwa wiki watakuwa wamekamilisha kazi ya kuweka mabati na kupiga plaster.

“Tunatarajia kukamilisha kazi ya ujenzi Mei 30, kama ilivyopangwa. Jengo lilikamilika litakuwa na kumbi mbili za mikutano na ofisi za kuchukua watumishi 88,” alisema.

Naye Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani alisema kuwa hadi sasa watumishi 73 kati ya 153 ndiyo wamehamia kwenye ofisi mpya za Mtumba. Alisema kwa sasa wanatenegeza eneo la maegesho ya magari na wameshatenga eneo la mgahawa kwa ajili ya wafanyakazi wa wizara hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages