A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, April 23, 2019

IS yadai kuhusika na mashambilizi ya Sri Lanka

Kundi la itikadi kali linalojiita "Dola la kiislam" IS, limedai kuhusika na mashambulio ya kujitoa mhanga maisha yaliyotokea makanisani na katika hoteli za kifahari na kuangamiza maisha ya zaidi ya watu 320 mnamo Jumapili ya Pasaka nchini Sri Lanka.

Kupitia shirika lake la kueneza propaganda, Amaq, kundi hilo limesema mashambulizi hayo yaliwalenga raia wa zile nchi zinazounda muungano dhidi ya IS pamoja na wakristo wa Sri Lanka.

Watu walioyatoa mhanga maisha yao walijiripua katika hoteli tatu za kifahari na makanisa matatu, wakati wa misa mjini Colombo na katika miji mengine ya Sri Lanka.

Waziri Mkuu wa Sri Lanka Ranil Wickremesinghe amesema mashambulizi hayo yana uhusiano na IS. Viongozi wa serikali wamewatwika jukumu la umwagaji damu huo, wanamgambo wa itikadi kali wa Thauheed Jamaath ambao mpaka sasa bado hawajatamka kama walikuwa nyuma ya mashambulio hayo au la.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages