A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, April 23, 2019

Waziri Mkuu akagua ofisi mpya za Wizara Saba


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekagua ofisi mpya za wizara saba katika mji wa Serikali ulioko Mtumba, Dodoma na kusisitiza waweke vibao vya ofisi na kukamilisha mazingira ya nje.

Ametoa agizo hilo leo jioni (Jumanne, Aprili 23, 2019) wakati akitoa majumuisho ya ziara hiyo fupi kwa maafisa wa Serikali waliokuwepo kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara ya nishati ambako ndiko alimalizia ziara yake.

“Kuna wizara hazina majina kwa nje. Hakikisheni majengo yote yanawekwa majina haraka ili kuondoa usumbufu kwa wananchi wanaokuja huku kutafuta huduma. Kama kuna wizara mbili ziko jirani, pale njia panda wekeni kibao kuonesha majina ya wizara zote mbili. Nia ya Serikaili ni kutoa huduma zote kutokea hapa Mtumba,” amesema.
Waziri Mkuu ametembelea wizara saba ambazo ni Maliasili na Utalii; Ofisi ya Rais - TAMISEMI; OWM - Sera, Uratibu na Bunge; Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora; Mifugo na Uvuvi, Ulinzi na JKT na ya mwisho ilikuwani ni Wizara ya Nishati.

“Nimefurahi kukuta Mawaziri, Naibu wao na Makatibu Wakuu pamoja na wakuu wa idara wako huku na kazi zinaendelea, lakini ni lazima nisisitize kwamba idara zinazohamia huku ziwe ni zile zenye kutoa huduma za kila siku kwa wananchi,” amesema.

“Ni lazima tuwaeleze wananchi na wadau wetu ili watambue kwamba Serikali imehamia huku, lakini wakija kutaka huduma wasikute idara inayowahusu iko mjini au wengine wako huku na wengine wako kule.”
Kuhusu miundombinu ya barabara, umeme na TEHAMA, Waziri Mkuu amesema Kamati ya Kitaifa ya kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma inasimamia kazi hiyo ikiwemo suala la ujenzi wa kituo kikubwa cha afya ambacho kitakuwa na huduma zote kwa viongozi lakini pia pia kitatoa huduma kwa wananchi waishio vijiji vya jirani.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages