A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, April 11, 2019

Simba SC yaahidiwa mamilioni ya fedha


Klabu ya Simba SC, imeambiwa itarajie kupokea kitita cha shilingi za kitanzania milioni 100 kutoka SportPesa endapo itafanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Pesa hizo Simba SC watazipata endapo tu watafanikiwa kuiondoa TP Mazembe kwenye hatua hiyo Jumamosi ya wiki hii.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Abbas Tarimba, amesema Simba watapokea mpunga huo kutokana na mkataba wao ambao walisaini nao unavyosema.

Ameeleza kuwa fedha hizo zitatolewa kama motisha ya kuzidi kuwafanya Simba wajitume vizuri zaidi kwenye mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages