A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, April 30, 2019

RC MAKONDA AWAPONGEZA WATENDAJI KWA KUSIMAMIA UKUSANYAJI MAPATO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza wakati wa mkutano wa  majumuisho kilichowakutanisha wakuu wa Wilaya, wakurugenzi, Makatibu Tawala, washauri wa miradi na wakandarasi  mkutano huo umefanyika leo jijini humo.
Baadhi ya wakurugenzi waliohudhuria mkutano huo.
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya waliohudhuria
Naibu Meya na Diwani wa Kata ya Vingunguti Omari Kumbilamoto, (kushoto), akifuatilia mkutano huo



MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amefanya kikao cha majumuisho kilichowakutanisha wakuu wa Wilaya, wakurugenzi, wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala, washauri wa miradi na wakandarasi na hiyo ni kufuatia ziara iliyofanywa na RC huyo katika kukagua miradi mbalimbali ya kimaendeleo jijini humo.


Akizungumza na watendaji hao Makonda amewapongeza watendaji kwa juhudi wanazozifanya katika kuleta maendeleo na kuwataka watimize ahadi zao kama walivyohaidi na hiyo hasa ni katika ujenzi wa vituo vya afya Buguruni na Kigogo kwa kuikamilisha kwa wakati huku akifurahishwa na kasi ya ujenzi wa hospitali za Wilaya za Ilala na Kigamboni ambazo zinajengwa kwa jumla ya shilingi bilioni 1.5 fedha ambazo zilizotolewa na Rais John Joseph Magufuli katika kuboresha sekta ya afya.


Aidha ameitaka Halmashauri ya Ubungo kuongeza kasi zaidi katika utatuzi wa kero za wananchi na kuwataka viongozi kuacha siasa na kuchapa kazi huku akielekeza nguvu zaidi iwekwe katika  shughuli za kimaendeleo.


Vilevile amewasisistiza wataalamu wa kusimamia miradi jijini humo kushirikisha wazawa katika miradi mikubwa ya kimaendeleo pindi tenda zinapotangazwa ili kuweza kuwainua na kuwapa fursa zaidi.


Wakati huo huo Makonda ametumia nafasi hiyo kuzipongeza halmashauri zote na watendaji wao kwa kuufanya Mkoa huo kuwa kinara katika ukusanyaji wa mapato kwa kipindi cha robo mwaka kwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 118.4 ikifuatiwa na Jiji la Dodoma lililokusanya  bilioni 57.3 na Jiji la Mwanza shilingi bilioni 22.9 huku Wilaya za Ilala na Kinondoni zikifanya vizuri zaidi nchini.


Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ilimulika miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika Wilaya zote jijini humo na katika ufanyaji wa tathimini hiyo viongozi na wasimamizi wa miradi hiyo wametakiwa kutimiza ahadi zao kwa kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.













No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages